Michael Kasaija
Michael Kasaija ni mwigizaji, mwanamitindo, mtengeneza dansi na mnenguaji kutoka Uganda.[1]Aliigiza kwa mara ya kwanza kama muigizaji mkuu kwenye filamu ya Bala Bala Sese ya mwaka 2015 akiwa na mchumba wake wa wakati huo Natasha Sinayobye.[2]
Maisha ya Mwanzo
[hariri | hariri chanzo]Michael alilelewa Kampala Uganda na alisoma Busoga College Mwiri na Caltec Academy.Akiwa Chuo kikuu cha Makerere , Michael alipata shahada ya usimamizi wa biashara na kushiriki katika mashindano na matamasha ya unenguaji na dansi.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Steve Jean alimuajiri Michael baada ya shule kuwa mnenguaji wake mkuu, kitu kilichomfikisha Michael kwa Pamela Basasirwaki, ambaye alianzisha nae mahusiano. Kama mwanachama wa kundi la dansi la Obsessions , Pamela alimtambulisha Michael kwenye kundi na alikubalika mara moja. Alikuja mnenguaji mwingine katika kundi , Natasha Sinayobye ambaye hakumhitaji tena na wawili hao waliondoka kwenye kundi 2005 na kuanzisha kundi lao la KOMBAT Entertainment Ltd.[3] Chini ya Kombat alifanikiwa kupata onyesho lake kubwa akitumbuiza katika sherehe za wakuu wa Nchi za CHOGM 52 zilizofanyika Uganda mwaka 2007. Hivi karibuni Michael alijipatia kazi kama meneja wa makundi machanga ya maigizo kwenye majaribio ya maonyesho , katika kipande cha tisa cha mfululizo wa maigizo ya usiku wa mahaba ya kundi.[4]Alikuwa pia mmoja wa majaji kwenye tamasha la NTV's Xp sambamba na wanamuziki , Isiah Katumwa, Jackie Chandiru na Bebe Cool.[5]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Kasaija ana mtoto wa kiume aitwae Sean Mario.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-03-05. Iliwekwa mnamo 2014-02-28.
{{cite web}}
: CS1 maint: archived copy as title (link) - ↑ Kamukama, Polly (2013-01-03). "The Observer - Kasaija, Natasha take romance to screen". Observer.ug. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-12-12. Iliwekwa mnamo 2013-03-04.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-16. Iliwekwa mnamo 2020-10-17.
- ↑ "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-03-05. Iliwekwa mnamo 2014-02-28.
{{cite web}}
: CS1 maint: archived copy as title (link) - ↑ http://www.monitor.co.ug/artsculture/Entertainment/Arua-has-got-talent/-/812796/2050674/-/mpwrraz/-/index.html
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michael Kasaija kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |