Bebe Cool
Moses Ssali (amezaliwa 1 Septemba 1977) ni mwanamuziki wa ragga kutoka nchini Uganda. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Bebe Cool. Alianza kazi yake kutoka 1997 akiwa Nairobi, Kenya, lakini miaka michache baadaye alirudi nchini kwake. Pamoja na Nameless na mwenzake Chameleone, Bebe Cool alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kujiimarisha na Ogopa DJs, nyumba ya uundaji muziki na studio nchini Kenya.
Nyimbo zake mbili maarufu ni "Fitina" na "Mambo mingi" [1] Yeye pia aliimba pamoja na Halima Namakula, msanii mwanamke kutoka katika wimbo wao "Sambagala". Alitoa albamu mbili, Maisha na Senta. Mistari ya nyimbo zake ziko katika Luganda, Kiswahili, na Kiingereza.
Bebe Cool ameshinda zawadi kadhaa katika Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) [2] Alikuwa ameteuliwa kwa Tuzo la Kora mwaka 2003 na 2005. Amezuru Uingereza na Marekani [3]
Pamoja na waimbaji wawili waKenya Necessary Noize, Bebe Cool ameunda kikundi cha reggae kinachojulikana kama East African Bashment Crew. Wametoa albamu moja, Fire, na nyimbo mbili, "Africa Unite" na "Fire". Kundi hili limeteuliwa katika uzinduzi wa (2008) MTV Africa Music Awards [4]
Bebe Kool ni mume wa aliyekuwa mshindani wa Miss Uganda Zuena Kirema na sasa ana watoto wawili.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Alishinda:
- 2004 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Msanii Bora wa Reggae / Kikundi [5]
- 2005 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Msanii Bora wa Reggae / Kikundi [6]
- 2006 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Msanii Bora wa Reggae / Kikundi [7]
- 2007 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Msanii Bora wa Reggae / Kikundi [8]
- 2008 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Msanii Bora wa Kiume na Msanii Bora wa Reggae / Kikundi na Kikundi Bora cha Ragga / Kikundi [9]
Ameteuliwa:
- Kora Awards 2003 - Msanii bora katika Afrika Mashariki [10]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ MTV Base Afrika: jsessionid = AMTFCT1IDES1TQFIAIICFE4AVABBCIV0? BackLink = profiler & id = 30119486 Artist profile - Bebe Cool (kupitia archive.org)
- ↑ [1] ^ Tovuti ya PAM Awards
- ↑ [2] ^ Musicuganda.com - Bebe Cool Archived 2012-09-05 at Archive.today
- ↑ ^ Museke: MTV Africa Music Awards 2008
- ↑ [4] ^ PAM Awards: Washindi wa 2004
- ↑ PAM Awards: 2005 Winners & Nominees
- ↑ Ugandaonline.net: PAM Awards 2006 Winners
- ↑ Museke: Pearl of Africa Music (PAM) Awards 2007 Washindi - Uganda Archived 26 Februari 2009 at the Wayback Machine.
- ↑ Museke: Pearl of Africa Music (PAM) Awards 2008 Washindi - Uganda Archived 5 Juni 2015 at the Wayback Machine.
- ↑ [7] ^ Kora Awards: Wateule 2003
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- [1] Archived 17 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Ngoni 2005 UGPulse.com Profile Archived 7 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- Musicuganda.com - Bebe Cool Archived 2012-09-05 at Archive.today