Nenda kwa yaliyomo

Methylphenidate

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Methylphenidate
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
Methyl phenyl(piperidin-2-yl)acetate
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Ritalin, Concerta, na mengineyo
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a682188
Taarifa za leseni US FDA:link
Kategoria ya ujauzito B3(AU) C(US)
Hali ya kisheria Controlled (S8) (AU) Schedule III (CA) ? (UK) Schedule II (US)
Uwezekano wa uraibu Juu[1]
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo, kupitia ngozi[1]
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili Takriban. 30% (kuanzia: 11–52%)
Kufunga kwa protini 10–33%
Kimetaboliki Ini (80%) mara nyingi kwa upatanishi waCES1A1
Nusu uhai Masaa 2–3[2]
Utoaji wa uchafu Mkojo (90%)
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Data ya kikemikali
Fomyula C14H19NO2 
Massi ya molekuli 233.31
Data ya kimwili
Kiwango cha kuyeyuka 74 °C (165 °F) [3]
Kiwango cha kuchemka 136 °C (277 °F) [3]
 YesY(Hiki ni nini?)  (thibitisha)

Methylphenidate, inayouzwa kwa jina la biashara Ritalin miongoni mwa mengineyo, ni dawa ya kusisimua inayotumiwa kutibu Tatizo la Kutotulia (ADHD) na ugonjwa wa usingizi kupindukia (Nakolepsia). Ni dawa ya mstari wa kwanza kwa ADHD.[1] Inaweza kuchukuliwa kwa mdomo au kutumika kwa ngozi.[1] Michanganyiko tofauti ina mida tofauti ya athari.[1]

Madhara ya kawaida ya methylphenidate ni pamoja na ugumu wa kulala, kupungua kwa hamu ya kula, wasiwasi na kupoteza uzito. Madhara yake makubwa zaidi yanaweza kujumuisha hali ya kuchanganyikiwa kiakili (psychosis), athari za mzio, kusimama kwa uume kwa muda mrefu, matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na matatizo ya moyo.[1] Methylphenidate inaaminika kufanya kazi kwa kuzuia uchukuaji upya wa dopamine na norepinephrine kupitia nyuroni.[4][5] Methylphenidate ni kichocheo cha mfumo mkuu wa neva (CNS) wa kundi la phenethylamine na piperidine.[1][6]

Methylphenidate ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1944 na iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1955.[7] Hapo awali iliuzwa na kampuni ya Uswizi ya CIBA, ambayo sasa ni Novartis Corporation.[7] Inakadiriwa kuwa katika mwaka wa 2013, dozi bilioni 2.4 za methylphenidate zilichukuliwa duniani kote. Mnamo mwaka wa 2017, ilikuwa dawa ya 47 inayoagizwa zaidi nchini Merika, ikiwa na maagizo zaidi ya milioni 16. Inapatikana kama dawa ya kawaida. [1] Nchini Marekani, gharama ya jumla ya uundaji wa kutolewa mara moja ni chini ya dola 0.30 kwa kila dozi kufikia mwaka wa 2018.

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named AHFS2018
  2. Kimko HC, Cross JT, Abernethy DR (Desemba 1999). "Pharmacokinetics and clinical effectiveness of methylphenidate". Clinical Pharmacokinetics. 37 (6): 457–70. doi:10.2165/00003088-199937060-00002. PMID 10628897.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Methylphenidate". Methylphenidate. National Center for Biotechnology Information. http://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/summary/summary.cgi?cid=4158#x27.
  4. Arnsten AF, Li BM (2005). "Neurobiology of Executive Functions: Catecholamine Influences on Prefrontal Cortical Functions". Biological Psychiatry. 57 (11): 1377–84. doi:10.1016/j.biopsych.2004.08.019. PMID 15950011.
  5. Stahl, Stephen M. (11 Aprili 2013). Stahl's Essential Psychopharmacology: Neuroscientific Basis and Practical Applications (tol. la 4th). Cambridge University Press. ISBN 978-1107686465.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Preedy, Victor R. (2016). Neuropathology of Drug Addictions and Substance Misuse Volume 3: General Processes and Mechanisms, Prescription Medications, Caffeine and Areca, Polydrug Misuse, Emerging Addictions and Non-Drug Addictions (kwa Kiingereza). Academic Press. uk. 651. ISBN 9780128006771. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2020.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 Lange KW, Reichl S, Lange KM, Tucha L, Tucha O (2010). "The history of attention deficit hyperactivity disorder". ADHD Attention Deficit and Hyperactivity Disorders. 2 (4): 241–55. doi:10.1007/s12402-010-0045-8. PMC 3000907. PMID 21258430.