Nakolepsia
Mandhari
Nakolepsia ni ugonjwa unaosababisha matatizo katika usingizi kwa kuathiri jinsi mishipa ya fahamu inavyofanya kazi.
Nakolepsia sio ugonjwa wa akili, au unaosababishwa na matatizo ya kisaikolojia.
Ugonjwa huo unatokea pale ambapo mfumo wa neva haufanyi kazi vizuri.
Wagonjwa wenye nakolepsia huwa na usingizi usiozuilika wakati wa mchana. Mara nyingi, hawapati usingizi mzuri usiku (wanapata usingizi wa mang'amung'amu), na wakati wa mchana wanalala bila kuweza kujizuia.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Maelezo ya kwanza yalitolewa mwaka wa 1877. Jean-Baptiste Gélineau, daktari wa kijeshi, alitumia jina la nakolepsia kwa mara ya kwanza mwaka wa 1880.
Katika baadhi ya nchi, wagonjwa wa nakolepsia, hawaruhusiwi kuendesha magari.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nakolepsia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |