Nenda kwa yaliyomo

Mercy Johnson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mercy Johnson Mnamo 2018

Mercy Johnson Okojie (alizaliwa Agosti 28, 1984) ni mwigizaji, mkurugenzi na mtayarishaji wa filamu wa Nigeria[1][2][3]. Alisoma elimu ya Sekondari /kkatika shule iitwayo River state na pai akasoma shule ya sekondari ya Navy huko Port Harcout katika Jimbo la River, Nigeria[4]. Baadaya ya kumaliza elimu yake ya Sekondari alienda kuigiza katika filamu inayoitwa The Maid na baadaye aliigiza katika filamu tofauti kama vile Hustlers, Baby Oku huko Marekani ma War in the Palace

Maisha ya Zamani

[hariri | hariri chanzo]

Mercy Johnson anatokea Okene katika Jimno la Kogi, lililoko katika ukanda wa kati wa nchi ya Nigeria. Alizaliwa katika mji wa Lagos, baba yake Daniel Johnson alikua ni afisa wa zamani wa Jeshi la Majini na mama yake alikua anaitwa Elizabeth, Mercy ni mtoto wa nne katika familia ya watoto saba. Alianza elimu ya shule ya msingi huko Calabar, katika Jimbo la Cross River lililopo kusini mwa Nigeria. Baba akiwa afisa wa Jeshi la Majini alihamishwa katika mji wa Lagos, Mercy aliendelea na elimu yake katika shule ya msingi ya Jeshi la wanamaji la Nigeria. Na baada ya hapo alisoma shule ya sekondari Rivers State kwa elimu ya sekondari na akajiunga na mafunzo ya wanajeshi wa maji huko Port Harcourt, River State.[5]

Baada ya kumaliza elimu yake ya Sekondari alienda kuigiza katika filamu inayoitwa The Maid na baadaye aliigiza katika filamu tofauti kama vile Hustlers, Baby Oku huko Marekani ma War in the Palace. Mwaka 2009, alishinda tuzo ya mwigizaji bora katika sherehe za African Movie Awards kutokana na uigizaji wake katika filamu ya "Live to Remember"[6][7]. Na tuzo ya mwigizaji bora katika tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards za mwaka 2013 kupitia filamu ya vichekesho inayoitwa Dumebi the Dirty Girl. Mnamo Desemba 2011, aliorodheshwa kama mtu maarufu wa Nigeria aliyetafutwa zaidi kwenye Google[8]. Mnamo Aprili 1, 2017 alipata cheo ya kua Msaidizi Mwandamizi Maalum wa Gavana wa Jimbo la Kogi katika burudani, sanaa na utamaduni.

Mercy Johnson alipigwa marufuku kuigiza kutokana na kua ghali sana mnamo Novemba 3, 2013, wataarishaji wa filamu wa Nollywood walimtishia kumzuia kwasababu ya kua na mahitaji makubwa[9]. Yeye na waigizaji wengine maarufu wa Nollywood kama vile Genevieve Nnaji, Omotola Jalade Ekeinde, Richard Mofe Damijo, Emeka Ike, Ramsey Nouah, Nkem Owoh, Stella Damasus na Jim Iyke walikatazwa kuigiza kwa madai ya kutaka kulipwa ela nyingi kwa kila filamu[10]. Hata hivyo marufuku hio iliondolewa na wataarishaji na wauzaji wa filamu mnamo Machi 9, 2014 baadaya ya Mercy Johnson kuomba msamaha[11].

Alikua mutaarishaji na muandaaji wa filamu iitwayo The Legend of Inikpi[12][13][14][15].

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Agosti 27, 2011, aliolewa na Prince Odianosen Okojie.[16][17]

  1. http://www.vanguardngr.com/2016/08/3-kids-3-years-needed-break/
  2. https://dailypost.ng/2016/08/21/get-busy-life-will-baby-number-4-mercy-johnson-blasts-critics/
  3. https://www.kemifilani.ng/entertainment/my-colleagues-are-waiting-to-hear-bad-news-from-me-mercy-johnson-okojie-spills
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-01-24. Iliwekwa mnamo 2024-04-16. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  5. "Mercy Johnson Biography, Life History, Profile & Movies - NaijaGists.com - Motivation, Faith, Natural Health & Relationship". naijagists.com (kwa American English). 2012-08-20. Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  6. "Mercy Johnson", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-03-20, iliwekwa mnamo 2024-04-16
  7. BellaNaija.com (2013-03-09). ""Otelo Burning" wins the Best Movie Award! View ALL the Winners from the AMVCA – 2013 Africa Magic Viewers' Choice Awards". BellaNaija (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  8. http://www.vanguardngr.com/2011/12/mercy-johnson-is-google-3rd-most-searched-celebrity/
  9. https://www.vanguardngr.com/2014/02/mercy-johnsons-ban-movie-marketers-break-silence/
  10. chibumga izuzu (2017-09-14). "13 years ago, 8 A-List actors were banned from Nollywood". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  11. Pulse Contributor (2014-03-17). "Movie Producers & Marketers Lift Mercy Johnson's Ban". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-16. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  12. Cyril (2020-01-08). "Mercy Johnson to release movie 'Legend of Inikpi' on Jan. 24". The Sun Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  13. Pulse Mix (2020-01-07). "Mercy Johnson releases trailer for "The Legend of Inikpi," movie to hit cinemas nationwide on January 24". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  14. "Mercy Johnson's 'Legend of Inikpi' - THISDAYLIVE". www.thisdaylive.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  15. Pulse Mix (2019-12-20). "Mercy Johnson releases teaser for 1st feature film as producer titled "The Legend of Inikpi"". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  16. Guardian Nigeria (2017-09-02). "Six years after marriage, Mercy Johnson still stands tall". The Guardian Nigeria News - Nigeria and World News (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-01-24. Iliwekwa mnamo 2024-04-16.
  17. https://www.vanguardngr.com/2019/08/i-suffer-pain-whenever-my-husband-is-upset-with-me-mercy-johnson-okojie/
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mercy Johnson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.