Melchior Ndadaye
Melchior Ndadaye (Machi 28, 1953 - Oktoba 21, 1993) alikuwa msomi wa sayansi na mwanasiasa. Yeye alikuwa wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia na wa kwanza wa kabila la Wahutu kuwa rais wa Burundi baada ya kushinda uchaguzi kuu wa kihistoria mwaka 1993.
Ingawa alijaribu kukomesha ukabila katika nchi hiyo, marekebisho yake yalishawishi askari katika jeshi lililotawaliwa na Watutsi, na aliuawa katikati ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa mnamo Oktoba 1993, baada ya miezi mitatu tu ofisini.
Kuuliwa kwake kulizua idadi ya mauaji ya kikatili baina ya makabila ya Watutsi na Wahutu, na mwishowe yalizua Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi vilivyodumu muongo mzima.
Mwaka 2020 mtangulizi wake Pierre Buyoya na wenzake wengi walihukumiwa kwenda jela maisha kwa kumuua[1]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Melchior Ndadaye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |