Nenda kwa yaliyomo

Pierre Buyoya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pierre Buyoya

Pierre Buyoya (Rutovu, Mkoa wa Bururi, 24 Novemba 1949 - Paris, Ufaransa, 18 Desemba 2020) alikuwa askari (meja) na mwanasiasa wa Burundi ambaye alitawala nchi mara mbili, kutoka mwaka 1987 hadi 1993 na kutoka 1996 hadi 2003. Kwa hiyo miaka 13 ya pamoja kama Mkuu wa Nchi, Buyoya ndiye Rais wa Burundi aliyeongoza muda mrefu zaidi.

Mwaka 2020 alihukumiwa kwenda jela maisha kwa kumuua mwandamizi wake, Melchior Ndadaye mwaka 1993[1], lakini kabla hajafungwa alifariki dunia kutokana na virusi vya Corona.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pierre Buyoya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.