Nenda kwa yaliyomo

Media Convergency

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Media Convergency Company Limited (Kwa kifupi MCC) ni Shirika lililopo mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania linayojishughulisha na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Pamoja na masuala ya kidigitali[1], shirika hili linafanya kazi na wadau wa maendeleo katika maeneo mbalimbali, shirika hili lilianzishwa tarehe 31 Agosti 2020 na Asha Daudi Abinallah[2]. Mbali na elimu ya kidigitali na intaneti, shirika hii linajishughulisha na mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni Mbali na elimu ya matumizi ya mitandao, Media Convergency wamekuwa wakifanya miradi ya kutoa elimu ya ufundishaji wasichana namna ya kujiepusha na vitendo vibaya kwa njia ya mtandao pamoja na kuwa elimisha vijana kuwa wabunifu wa kidigitali. Asasi hii hushughulika na kufanya Uchechemuzi wa mambo mbalimbali kwa njia ya mtandao wa kijamii na ana kwa ana.

Women at Web

[hariri | hariri chanzo]

Media Convergency inatekeleza mradi wa Women at Web ,mradi huu ulianza mwaka 2018 na kuanzishwa na DW Akademie , mradi huu unatekelezwa katika nchi nne za Afrika ya Mashariki ambazo ni Tanzania [3],Kenya, Rwanda na Uganda ukiwa na malengo ya kuwahamasisha na kuwajengea uwezo wasichana na wanawake katika kujiingiza na kujikita katika matumizi ya Kidigitali na Internet. [4]

The Innovation and Tech Forum

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 27 Agosti 2021,Media Convergency kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania kupitia UNDP walizindua mradi wa Jukwaa la Ubunifu katika Teknolojia kupitia Buni Innovation Hub kwa malengo ya kuendeleza ubunifu katika teknolojia, kuwaunganisha wabunifu pamoja na kuwakutanisha pamoja wabunifu wadogo na wabunifu wakubwa.


  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-22. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.
  2. "Asha D. Abinallah". Media Convergency (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-05-28. Iliwekwa mnamo 2022-05-25.
  3. https://womenatweb.co.tz/
  4. https://www.dw.com/en/as-members-of-womenweb-two-women-in-rwanda-and-tanzania-strive-to-empower-women-and-enhance-their-participation-in-the-digital-sphere/a-61363211