Asha Daudi Abinallah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Asha Daudi Abinallah Maarufu kama AshaDii ni mwanamke Mtanzania na mkurugenzi wa shirika la Media Convergency linalojihusisha na TEHAMA kutatua changamoto mbalimbali za kidijitali. Asha amebobea katika kutoa ushauri wa vyombo vya habari na uandishi, mhamasishaji wa vijana. Pia anafundisha jamii kuhusu ufahamu wa jinsia na matumizi ya mitandao ya kijamii.[1]

Asili

Asha Abinallah amezaliwa 23 Juni, 1981 mkoani Mbeya uliopo nyanda za juu kusini mwa Tanzania na ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya mzee Daudi Abinallah. Amefanikiwa kupata watoto wawili na alifanikiwa kurudi shule baada ya kupata mtoto akiwa kidato cha nne.

Masomo

Asha Abinallah alihitimu masomo yake ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo alichukua Shahada ya Medical Sociology and Archaeology.

Mwaka 2019 alifanya kozi ya mwaka mmoja maendeleo ya habari kwenye mfumo wa demokrasia kutoka kwenye taasisi ya fojo iliyo chini ya chuo kikuu cha Linnaeus nchini Sweden.

Mwaka 2020, Asha alihitimu shahada ya uzamili kwenye 'New Media' kutoka chuo kikuu cha Leeds nchini Uingereza

Taaluma

Safari ya Asha Abinallah kwenye dunia ya Tehama ilianza alipojiunga na kampuni ya Jamii Media mwaka 2011 iliyomiliki mtandao wa Jamii Forums na Fikrapevu[2]

Mwaka 2020 Asha Abinallah alifanikiwa kuanzisha kampuni ya Media Convergency, inajihusisha na TEHAMA na kupitia ubunifu wa teknolojia inasuluhisha changamoto mbalimbali za kidijitali ikiwemo kutumia taarifa na teknolojia kupata majibu yenye tija kwenye dijitali.

Pia Asha Abinallah anafanya kazi na DW Akademie kwenye mradi wa women at web ukilenga kuwawezesha wanawake na wasichana kutumia intanet kwenye maendeleo yao ya kiuchumi[3] Asha alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya Jamii Media ambayo anamiliki JamiiForums.com na FikraPevu.com[4].Pia ni mwandishi wa vitabu akiwa na kitabu chake cha siasa kitwacho Asemavyo Zitto[5].

Pia ni mwandishi wa vitabu akiwa na kitabu chake cha siasa kitwacho Asemavyo Zitto[6].

Mafanikio

Asha Abinalla alifanikiwa kupata tuzo ya uongozi 2022 kwenye wanawake katika utawala Afrika-STEM[7]

Asha alifanikiwa kushiriki kama mmoja wa 2015 Mandela Washington Fellows.

Marejeo

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asha Daudi Abinallah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.