Meddie Kagere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Meddie Kagere (alizaliwa 10 Oktoba 1986) ni mchezaji wa soka wa Rwanda aliyezaliwa Uganda ambaye anacheza katika klabu ya Simba S.C. iliyopo Ligi Kuu Tanzania Bara na timu ya taifa ya Rwanda.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

KF Tirana[hariri | hariri chanzo]

Kagere alijiunga na klabu yake ya kwanza huko Ulaya wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya joto 2014, alipojiunga na Albania Superliga katika klabu ya KF Tirana baada ya mkataba wa miaka miwili kuisha alirudi katika klabu yake ya awali ya Rayon Sports FC ya kwa $ 10,000. Mnamo 1 Januari 2015, Kagere alitolewa na KF Tirana na kujiunga na Gor Mahia ya Kenya.

Simba S.C.[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kufanya vizuri katika mwaka 2018 SportPesa Super Cup, wakati alikuwa mchezaji wa Gor Mahia F.C, alifunga goli la kwanza dhidi ya Simba S.C., hatimaye alisajiliwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Simba S.C. Katika msimu wa 2019/20 ni mmoja kati ya wachezaji bora.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meddie Kagere kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.