Mbilia Bel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbilia Bel

Mbilia Bel (kwa jina la kuzaliwa anaitwa Marie-Claire Mboyo Moseka; amezaliwa 10 Januari 1956) ni mwanamuziki katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mbilia Bel alianza kazi ya muziki akiwa na miaka kumi na saba, akiwa mwimbaji pia mchezaji kwa mwanamuziki Abeti Masikini. Aliimba nyimbo nyingi za mwanamuziki Bella Bellow, kisha, akaungana kwa nyimbo na mwanamuziki Sam Mangwana.

Amekuwa mwanamuziki maalumu katika nchi ya Kongo kwenye mwanzo wa mwaka 1980, wakati alipoingia katika Afrisa International ya Tabu Ley Rochereau.