Matumizi sahihi ya dawa
Matumizi sahihi ya dawa ni kufuata kanuni, taratibu na maelekezo yote sahihi kutoka kwa tabibu wa afya. Hivyo basi tabibu akimpa mtumia dawa za ugonjwa fulani, mgonjwa huyo hana budi kufuata maelekezo hayo kama yanavyomtaka atumie.
Kwa kawaida matumizi ya dawa yapo katika namna mbalimbali; kuna kila baada ya saa 24,12, na 8
Kwa mfano : Matumizi kila baada ya saa 24.
1 x 1,
2 x 1,
3 x 1,
4 x 1.
Matumizi kila baada ya saa 12.
1 x 2,
2 x 2,
3 x 2,
4 x 2.
Matumizi kila baada ya saa 8.
1 x 3,
2 x 3,
3 x 3,
4 x 3.
Hivyo basi mtumiaji wa dawa tiba akienda kinyume na matumizi sahihi ya dawa kwa mujibu wa tabibu anaweza kukumbwa na athari mbalimbali mfano kupoteza uhai, kudhoofika kwa mwili, na kuibua aina nyinginezo za magonjwa kama vile kansa.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matumizi sahihi ya dawa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |