Maryse Condé

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maryse Condé mnamo 2008
Maryse Condé mnamo 2008

Maryse Condé (née Boucolon; 11 Februari 1937) ni mwandishi wa riwaya na wa maigizo wa Ufaransa, pia mkosoaji, kutoka Eneo la ng'ambo la Ufaransa na mkoa wa Guadeloupe.

Condé anafahamika zaidi kwa riwaya yake ya Ségou (1984–85). [1]

Riwaya zake zinachunguza diaspora ya Waafrika iliyotokana na utumwa na ukoloni uko Karibiani. Riwaya zake, zilizoandikwa kwa lugha ya Kifaransa, zimetafsiriwa kwa Kiingereza, Kijerumani, Kiholanzi, Kiitaliano, Kihispania, Kireno na Kijapani. [2] Ameshinda tuzo mbalimbali, kama vile Grand Prix Littéraire de la Femme (1986), Prix de l'Académie française (1988), Prix Carbet de la Carraibe (1997) [3] na New Academy Tuzo katika Fasihi (2018) kwa kazi zake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Condé, Maryse, and Richard Philcox. Tales from the Heart: True Stories from My Childhood. New York: Soho, 2001.
  2. Maryse Condé | Columbia | French. french.columbia.edu. Iliwekwa mnamo 2019-03-16.
  3. "Author Profile: Maryse Condé". World Literature Today (September–December 2004), 78 (3/4), p. 27.
Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maryse Condé kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.