Nenda kwa yaliyomo

Mark Randall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mark Randall
Maelezo binafsi
Jina kamili Mark Randall
Tarehe ya kuzaliwa 28 Septemba 1989
Mahala pa kuzaliwa    Milton Keynes, Uingereza
Urefu 1.83m
Nafasi anayochezea Mchezaji wa kati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 48
Klabu za vijana
1999-2001 Northampton Town
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2008 Burnley katika mpango wa mkopo
Timu ya taifa
Uingereza

* Magoli alioshinda

Mark Leonard Randall (alizaliwa Milton Keynes, 28 Septemba 1989) ni mchezaji wa Uingereza anayecheza kama mchezaji wa kati anayelinda ama mchezaji wa upande wa kulia wa kati.

Randall alitia saini mkataba na Arsenal kwa fomu ya aina ya vijana wa shule.Akacheza mechi saba katika Ligi Kuu ya Timu Hifadhi katika msimu wa 2005-2006. Randall pia alikuwa mchezaji pekee katika timu aliyecheza katika mechi yote 18 ya timu hifadhi katika msimu wa 2007-08. Yeye alicheza katika mechi ya makumbusho ya Dennis Bergkamp dhidi ya Ajax Amsterdam katika mwezi wa Julai 2006 na pia katika michuano ya kabla ya msimu huko nchini Austria na Uholanzi. Yeye alichezea timu ya kwanza kwa mara ya kwanza alipoingia kama mchezaji mbadala katika mechi dhidi ya West Bromwich Albion ya Shindano la Kombe la League katika tarehe 25 Oktoba 2006. Yeye ,pia, alicheza katika mechi ya Arsenal dhidi ya Everton mnamo 8 Novemba 2006,akiwa mchezaji mbadala kwa Denilson.Vilevile,alikuwa ameorodheshwa kama mojawapo wa wachezaji ambao wangeingia baadaye katika robo fainali yao dhidi ya Liverpool-lakini hakucheza katika mechi hiyo. 's nne-duru mechi dhidi ya Everton tarehe 8 Novemba 2006, tena kuja juu kwa Denílson, na alikuwa kwenye benchi kwa robo fainali dhidi ya Liverpool, lakini hakuwa na kucheza katika mechi.

Tarehe 8 Februari 2007, alipiga saini mkataba na Arsenal na katika majira ya joto ya 2007 alishiriki katika kambi ya kufanya mazoezi kabla ya msimu kuanza ya Arsenal nchini Austria. Hata hivyo,hakucheza kwa miezi kadhaa ya mwanzo wa msimu wa 2007-2008 baada ya kupata jeraha katika mechi ya kwanza ya timu hifadhi ya Arsenal katika ligi yao.Hata hivyo,aliwez kuchezea timu ya kwanza katika mechi ya robo fainali katika Shindano la kombe la League dhidi ya Blackburn Rovers mnamo 18 Desemba 2007.Alicheza tena katika shindano hilo kama mchezaji mbadala katika nusu fainali dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Randall alipiga saini mkataba wa mkopo na Burnley tarehe 31 Januari 2008,katika siku ya mwisho ya kuhamisha wachezaji na akacheza mechi 10 katika timu ya Burnley. Alirudi Arsenal katika mwisho wa msimu tarehe 4 Mei na akacheza katika mechi yake ya kwanza katika Ligi Kuu dhidi ya Sunderland tarehe 11 Mei-mechi ya mwisho ya Arsenal ya msimu. Yeye aliingia katika mechi hiyo kama mchezaji mbadala katika dakika 81 na bao moja lake likakataliwa katika dakika za mwisho wa mechi.

Mark Randall aking'ang'ania mpira na mchezaji wa timu pinzani.

Baada ya kucheza katika mechi mengi ya kabla msimu ya 2008-09,Randall alicheza katika mechi yake ya kwanza ya Uropa katika mechi ya Arsenal na FC Twente mnamo 13 Agosti 2008.Aliingia kama mchezaji mbadala wa Theo Walcott. Alicheza pia dakika zote 90 katika mechi ya Shindano la Kombe la League dhidi ya Sheffield United mnamo 23 Septemba.Mechi hiyo iliisha 6-0,huku Randall akipanga mchezo mzuri uliosababisha kufungwa kwa bao la tano na Jack Wilshere. Alicheza pia katika mechi walioshinda 3-0 dhidi ya Wigan Athletic.Vilevile alicheza katika robo fainali ambayo walishindwa na Burnley. Alicheza kwa mara ya kwanza katika Shindano la Ligi ya Mabingwa mnamo 10 Desemba alipoingia kama mchezaji mbadala wa Alexander Song waliposhindwa 2-0 na timu ya Porto.

Msimu wa 2009/10

[hariri | hariri chanzo]

Randall alishiriki katika ushindi dhidi ya West Bromwich Albion katika Shindano la Kombe la League akiwa mchezaji mbadala wa Francis Coquelin katika dakika ya 58.

Takwimu ya Wasifu akiwa Arsenal

[hariri | hariri chanzo]

Sahihi tangu 10 Oktoba 2008.

Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Kombe la League Uropa Jumla
Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wake katika mechi Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wake katika mechi Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wake katika mechi Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wake katika mechi Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wake katika mechi
Arsenal 2006–07 0 0 0 0 0 0 2 0 0 0 0 0 2 0 0
Arsenal 2007–08 1 0 0 0 0 0 2 0 0 0 0 0 3 0 0
Burnley (mpango wa mkopo) 2007–08 10 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 10 0 0
Arsenal 2008–09 1 0 0 0 0 0 3 0 0 2 0 0 5 0 0
Arsenal 2009–10 0 0 0 0 0 0 2 0 0 0 0 0 2 0 0
  1. West Brom 0-2 Arsenal, bbc.co.uk.
  2. Everton 0-1 Arsenal, bbc.co.uk.
  3. Randall apiga saini mkataba, arsenal.com
  4. Randall na mkataba mpya!, arsenal.com.
  5. Blackburn 2-3 Arsenal (aet), bbc.co.uk.
  6. Arsenal na Spurs, skysports.com.
  7. Arsenal 1-1 Tottenham, bbc.co.uk.
  8. Kuhusu Randall Archived 12 Aprili 2008 at the Wayback Machine., burnleyfootballclub.com.
  9. Walcott ashindia Gunners, skysports.com.
  10. FC Twente 0-2 Arsenal Archived 28 Agosti 2008 at the Wayback Machine., arsenal.com.
  11. - Arsenal 3-0 Wigan , BBC Sport.
  12. - Burnley 0-2 Arsenal , BBC Sport.
  13. [1], uefa.com.
  14. Arsenal 2-0 W.B.A Archived 16 Desemba 2013 at the Wayback Machine. arsenal.com.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]