Nenda kwa yaliyomo

Marianne Koch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marianne Koch
Koch akiwa na Clint Eastwood katika filamu ya A Fistful of Dollars (1964).
Koch akiwa na Clint Eastwood katika filamu ya A Fistful of Dollars (1964).
Jina la kuzaliwa Marianne Koch
Alizaliwa 19 Agosti 1931,
Ujerumani
Kazi yake Mwigizaji, daktari
Miaka ya kazi uigizaji 1950-1970
tiba 1974-1997
Ndoa 1953 - 1973 na Gerhard Freund
Watoto wavulana 2

Marianne Koch (amezaliwa tar. 19 Agosti 1931) ni daktari wa tiba na mwigizaji filamu mstaafu wa Ujerumani, aliyecheza filamu kati ya miaka ya 1950 na 1960, anafahamika zaidi kwa mwonekano wake katika filamu za western ya Italia, maarufu kama spaghetti westerns, na filamu za kipelelezi za miaka ya 1960.

Marianne ameonekana katika zaidi ya filamu 65 kati ya mwaka 1950 na 1970 zikiwemo na filamu ziliongozwa na Sergio Leone, ambayo ni "A Fistful of Dollars" ya mwaka 1964 ambayo ndio picha inayoneka amekaa na Clint Eastwood.

1970 alipokuwa na umri wa miaka 39 akaamua kuacha uigizaji filamu akarudi chuo kikuu na kumaliza masomo yake ya tiba. 1974 akapata cheo cha daktari na kuanzisha kliniki yake ya tiba ya ndani mjini München. Alistaafu 1997. Ana watoto wawili wa kiume.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marianne Koch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.