Nenda kwa yaliyomo

Mariana Ochoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mariana Ochoa
Mariana Ochoa.
Mariana Ochoa.
Jina la kuzaliwa Mariana Yolanda Ochoa Reyes
Alizaliwa 19 Februari 1979
Mexiko
Jina lingine Mariana Ochoa
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamuziki

Mariana Yolanda Ochoa Reyes (amezaliwa Mexico City, Mexico, 19 Februari 1979) ni muigizaji wa filamu na mwanamuziki kutoka nchi ya Mexico.

Alikuwa mwanachama wa kundi la muziki maarufu kama OV7 (awali lilifahamika kama La Onda Vaselina). Baada ya kuachana, Ochoa alianza kujitangaza mwenyewe katika masuala ya muziki na uigizaji.

Wasifu

Maisha ya filamu na muziki

Tamthilia yake kwanza kumpa umaarufu na kukubalika kwa Mariana ilikuwa La Hija Del Jardinero, iliyo andaliwa na TV Azteca production. Tamthilia hiyo ilipokelewa vizuri tu huko Latini Amerika.

Hivi karibuni Mariana alitoa tamthilia nyingine nzuri ya kuvutia iitwayo "Amor Sin Condiciones" na kuweza kuipiku hata ile ya 'Secreto de Amor' ambayo iliandaliwa mwaka 2001 na kampuni ya Venevisión wakishirikiana na Fonovideo ya Miami nchini marekani.

Pamoja Ochoa na kushughulika na kurekodi albamu yake ya pili lakini bado pia anashughulika na kurekodi tamthilia mpya itakayo rushwa hewani na TV Azteca, tamthilia inaitwa "Se Busca un Hombre" ambayo pia inaandaliwa na kampuni ya TV Azteca.

Albamu alizotoa

Albamu Mwaka Studio
Yo Soy 2004 EMI Music
Luna Llena 2007 Warner Music


Mnamo mwezi Machi, 2006, Ochoa amebadilisha studio ya EMI na kuhamia Warner Music kwa mkataba wa kurekodi kwa muda wa miaka kumi.
Mwezi Julai, 2007, Ochoa alirekodi albamu yake ya pili iliyoitwa Luna Llena.

Nyimbo maarufu

  • My Lover
  • Deseos
  • Qué Importa
  • Me Faltas Tú (#20 - EXA Guatemala
  • Aunque No Estés (Kwa Ushirikiano wa Alex Ubago)

Marejeo

  1. http://www.emimusic.com.mx/portal/hgxpp001.aspx?2,114,23,O,S,0,MNU;E;72;7;MNU Archived 29 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.;
  2. "Como Nunca Existió" Archived 11 Januari 2007 at the Wayback Machine.
  3. http://foro.univision.com/univision/board/message?board.id=mariana_ochoa&message.id=78515
  4. Ochoa Kwenye 10 Bora

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mariana Ochoa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.