Marekani (kitambaa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa marekani (calico) pamoja na futi.

Marekani (pia: merekani, merikani) ni kitambaa kizito cha pamba kisichotiwa rangi.

Jina hilo lilianza kutumiwa katika miaka ya 1835 wakati meli kutoka Marekani zilianza kufika kwenye pwani za Afrika ya Mashariki wakitafuta hasa pembe ya ndovu na kuleta kitambaa cha kwao. Kitambaa hicho kiliuzwa kwa bei nafuu na kuwa imara zaidi kuliko vitambaa vya Uhindi na Uingereza ambavyo vilifika kwenye miji ya Waswahili hadi wakati ule[1]. Kwa hiyo watu waliita kwa jina la nchi ilipotoka, Marekani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Abdul Sheriff: Slaves, Spices, and Ivory in Zanzibar: Integration of an East African Commercial Empire into the World Economy, 1770-1873 (Eastern African Studies), Ohio University Press (September 30, 1987), ISBN-10: 0821408720 ISBN-13: 978-0821408728, uk. 95