Nenda kwa yaliyomo

Marc Andre ter Stegen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Golikipa wa timu ya klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Ujerumani.

Marc André ter Stegen (alizaliwa 30 Aprili 1992) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Ujerumani. Anacheza kama golikipa wa klabu ya Barcelona FC na timu ya taifa ya Ujerumani.

Baada ya majira manne katika Bundesliga na Borussia Dortmund, alijiunga na Barcelona kwa milioni 12 mwaka 2014. Alipata vikombe vinne katika msimu wake wa kwanza nchini Hispania. Kucheza kwa Barcelona ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA) kumempelekea Ter Stegen kupata umaarufu na kuwa golikipa bora wa msimu wa kwanza.

Barcelona FC[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 19 Mei 2014, Ter Stegen ulitangazwa kuwa golikipa mpya wa klabu ya Barcelona FC, baada ya uondokaji wa Victor Hipolito Valdés na José Manuel Pinto. Ter Stegen alisaini mkataba wa miaka mitano ambayo inamzuia kuhama hadi Juni 2019.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marc Andre ter Stegen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.