Manu Dibango

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Emmanuel N'Djoké (Manu" Dibango) (12 Desemba 1933 - 24 Machi 2020) [1] alikuwa mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo kutoka Kameruni ambaye alicheza saksafoni na vibraphone . Alianzisha mtindo wa muziki wa kuchanganya jazba, funk, na muziki wa kitamaduni wa Kameruni. Baba yake alikuwa mwanachama wa kabila la Yabassi, wakati mama yake alikuwa Duala . Alijulikana zaidi kwa wimbo wake wa 1972 " Soul Makossa ". Alikufa kutokana na COVID-19 tarehe 24 Machi 2020. [2] [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Le saxophoniste Manu Dibango est mort des suites du Covid-19, annoncent ses proches". 
  2. Beaumont-Thomas (24 March 2020). Manu Dibango, Cameroon jazz-funk star, dies aged 86 of coronavirus. The Guardian. Iliwekwa mnamo 5 May 2020.
  3. Monroe (24 March 2020). Afro-Jazz Star Manu Dibango Dead at 86. Pitchfork (website). Iliwekwa mnamo 24 March 2020.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Manu Dibango kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.