Mansa Musa
Mansa Musa (1280-1337) alikuwa mtawala tajiri wa Mali ya Magharibi.
Ufalme wa Mali ulikuwa na eneo la zamani la Ufalme wa Ghana kusini mwa Mauritania na Melle (Mali) na maeneo yaliyo karibu.
Jina lake pia linaonekana kama Kankou Musa, Kankan Musa, na Kanku Musa. "Kankou" ni jina maarufu la kike. Musa alikuwa na majina mengi, yakiwa ni pamoja na "Emir wa Melle", "Bwana wa Mines ya Wangara", "Mshindi wa Ghanata".
Mansa Musa aliishinda miji 24. Wakati wa utawala wake (1312–1337), Mali iliweza kuwa na uzalishaji mkubwa wa dhahabu duniani; ilikuwa wakati ule ambao kulikuwa na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo. Alikuwa mmoja wa watu tajiri zaidi katika historia; gazeti la Time liliripoti: Hakika hakuna njia ya kutathmini kwa usahihi utajiri wake.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mansa Musa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |