Maliki Junubi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maliki Junubi (A Leonis, Regulus)
(mfumo wa nyota 4, tatu zinatambuliwa)
Kundinyota Asadi (pia: Simba, Leo)
Mwangaza unaonekana 1.4 / 8.13 / 13.5
Kundi la spektra B8 IV / K2 V / M4 V
Paralaksi (mas) 41.13 ± 0.35
Umbali (miakanuru) 80
Mwangaza halisi -0.57 / 6.3 / 11.6
Masi M☉ 3.8 / 0.8 / 0.3
Nusukipenyo R☉ 3092 / 0.5 / ?
Mng’aro L☉ 288 / 0.5 / ?
Jotoridi usoni wa nyota (K) 12,460 / 4885 / ?
Muda wa mzunguko siku 15-16
Majina mbadala α Leonis, Alpha Leonis, 32 Leo, Cor Leonis, Aminous Basilicus, Lion’s Heart, Rex, Kalb al Asad, Kabeleced, FK5 380, GCTP 2384.00, GJ 9316, HIP 49669, HR 3982


Maliki Junubi (Regulus) katika makundinyota yake ya Asadi – Leo jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji wa Afrika ya Mashariki

Maliki Junubi (ing. na lat. Regulus pia α Alfa Leonis, kifupi Alfa Leo, α Leo) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Simba (pia Asadi, lat. Leo).

Jina

Maliki Junubi inayomaanisha “Mfalme wa Kusini” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema المليك al-malik linalomaanisha "mfalme". Waarabu waliwafuata hapa Wagiriki wa Kale waliosema βασιλίσκος basiliskos (mfalme mdogo). Jina mbadala lilikuwa “moyo wa simba” yaani قلب الأسد qalb al-asad. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali umbo la Kilatini la jina na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Regulus" [2] (yaani mfalme mdogo).

Alfa Leonis ni jina la Bayer maana ina nafasi ya kwanza kufuatana na mwangaza katika kundinyota yake.

Tabia

Maliki Junubi - Regulus iko umbali wa miakanuru 77.5 kutoka Jua letu. Ina mwangaza unaoonekana wa 1.36 na mwangaza halisi ni -0.2. Spektra yake ni ya aina ya B7.

Iko angani karibu na mstari wa ekliptiki, hivyo inafunikwa mara nyingi na Mwezi.

Maliki Junubi ni mfumo wa nyota maradufu nne au labda zaidi. Nyota kuu ni Regulus A iliyo na rangi ya buluu-nyeupe na masi ya 3.5 Inafuatana na nyota kibete nyeupe yenye masi ya M☉ 0.3 na zote mbili zinazunguka kwa pamoja kitovu chao cha graviti katika muda wa takriban siku 40.[3].

Nyota mbili nyingine ya mfumo huu zinaitwa B na C zikiwa umbali wa vizio astronomia 5,000 kutoka A.

Tanbihi

  1. ling. Knappert 1993
  2. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  3. Rappaport, S.; Podsiadlowski, Ph.; Horev, I. (2009)

Viungo vya Nje


Marejeo

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 59 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Perseus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
  • Rappaport, S.; Podsiadlowski, Ph.; Horev, I. (2009). "The Past and Future History of Regulus". The Astrophysical Journal. 698 (1): 666–675 online hapa
  • Gies, D.R.; Dieterich, S.; Richardson, N. D.; Riedel, A. R.; Team, B. L.; McAlister, H. A.; Bagnuolo, Jr., W. G.; Grundstrom, E. D.; Štefl, S.; Rivinius, Th.; Baade, D.; et al. (2008). "A Spectroscopic Orbit for Regulus". The Astrophysical Journal. 682 (2): L117–L120. online hapa