Makubi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Makubi ni aina ya kitoweo ambayo uleta ladha wakati wa kula.

Hiyo mboga hupikwa kwa kutumia vitu vifuatavyo: nyama ya kusaga, spinachi, kitunguu, karoti na nyanya.

Namna ya kupika[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kupika kwanza unachemsha nyama yako, halafu unaandaa vitu vilivyotajwa hapo juu; ukishamaliza unawasha moto wako au gesi yako, halafu unatenga sufuria yako jikoni. Hapo unaanza kupika: cha kwanza kabisa katika mapishi yetu unaanza kuweka mafuta, unaacha yapate moto kidogo. Baada ya hapo unaweka vitunguu; hivyo vitunguu unaacha mpaka viwe vya kawahia. Baada ya hapo unaweka nyanya, nazo unaziacha mpaka zilainike. Ukishamaliza unaweka nyama yako uliyoisaga, unaacha vichemke mpaka nyama itakapoiva. Ukishamaliza unaweka spinachi yako, halafu unaigeuza kidogo, halafu unaiacha ichemke. Na wakati inapochemka hayatakiwi maji mengi: yenyewe inatakiwa iwe nzito. Hapo mboga imeshakwishaiva, unaiweka kwenye chombo safi, baada ya hapo ipo tayari kwa kula. Hii ni njia fupi ya kupika makubi.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makubi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.