Maji ya Chai

Majiranukta: 3°20′43.8″S 36°53′52.6″E / 3.345500°S 36.897944°E / -3.345500; 36.897944
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

3°20′43.8″S 36°53′52.6″E / 3.345500°S 36.897944°E / -3.345500; 36.897944

Maji ya Chai ni kata ya Wilaya ya Meru katika Mkoa wa Arusha, Tanzania, yenye postikodi namba 23302.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 19,779 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 29,313 [2] walioishi humo.

Kata iko mguuni pa Mlima Meru kwa kimo cha mita 1,269 juu ya usawa wa bahari.[3]

Sehemu hii ilipewa jina hili kutokana na maji ya mto unaopita humo.[4] Rangi yake ni kama chai ambayo hupikwa kwa kuchemsha maji na majani kuleta rangi nyeusi-kahawia.

Rangi hii inatokana na kemikali zilizopo katika ardhi ya mazingira ya Mlima Meru, hasa bikabonati HCO3 na bikabonati natiri (magadi Na2CO3) ambazo zinarahisisha kuyeyusha kwa mata ogania kutoka sehemu za matopematope ambako mto unapita[5] na kuingia katika maji ya mto[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Arusha - Meru DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-21. 
  3. linganisha Tovuti ya Mapcharte, Maji ya Chai
  4. Background of Imbaseni Village, tovuti ya Imbaseni org, iliangaliwa tar. 1 Julai 2017
  5. Kwa hiyo rangi haitoki moja kwa moja kutoka kwa magadi na bikabonati mabli ni rangi nyeusi ya mata ogania inayoyeyushwa na maji yenye magadi
  6. "The brown colour of the Maji-ya-Chai, and the red colour of the Engare Nanyuki-the origin of both their names-appear to be due simply to the fact tha.t these alkaline rivers pass through, or receive seepage from, swamps containing much humic material readily soluble in alkali." CHEMICAL SURVEY OF THE WATERS OF MOUNT MERU, TANGANYIKA TERRITORY, ESPECIALLY WITH REGARD TO THEIR QUALITIES FOR IRRIGATION uk. 26, taarifa ya Sturdy (Department of Agriculture, Tanganyika), Calton na Milne, Journal of East African Natural History 1-1932, kwenye tovuti ya http://www.biodiversitylibrary.org.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Meru - Mkoa wa Arusha - Tanzania

Akheri | Ambureni | Imbaseni | Kikatiti | Kikwe | King'ori | Leguruki | Majengo | Maji ya Chai | Makiba | Malula | Maroroni | Maruvango | Mbuguni | Ngabobo | Ngarenanyuki | Nkoanekoli | Nkoanrua | Nkoaranga | Nkoarisambu | Poli | Seela Sing'isi | Shambarai Burka | Songoro | Usariver | Uwiro


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maji ya Chai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.