Majadiliano ya mtumiaji:Mzee Samwel Musika

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mzee Samuel Musika Warioba alizaliwa tarehe 01/04/1918 asili yake kikiwa huko Nyamang'uta kijiji cha Sarawe. Mzee Musika alikuwa ni mtoto wa tano kuzaliwa kutoka kwenye tumbo la mama yake aitwae Nzota Nyakabha. Watoto wengine wa Nzota (Mama yake na Samuel) ni; Nyamata (Dada yao wapekee), Masudi, Ibhoka na Mogonya.

Mzee samuel Musika katika maisha yake ya utafutaji alihama kutoka Nyamng'uta na kuhamia kijiji cha bukama kilichopo wilaya ya Bunda mkoani Mara Tanzania.

Mzee Samuel Musika alisomea shule za misheni (Mission) za kisabato.

Mzee Samuel Musika alijihususha na shughuli za Ukulima, Ufugaji na biashara katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, Nchini Kenya, Uganda na nchi nyingine za Afrika mashariki. Shughuli hizi zilimsaidia kupata mafankio makubwa sana kimaisha.

Mzee Samuel Musika alioa wanawake watatu Rahabu Daudi (Nyabhanane), Nyakatende, Nyawanzagi na kwa wake zake wote alibahatika kupata watoto 27, wajukuu 68+ na vitukuu 78+.

Kabla ya kufariki Mzee Samuel Musika alipoteza wake zake wawili, Nyabhanane na Nyakatende pamoja na watoto 14 na wajukuu wawili.

Kutokana na shughuli alizokuwa nazo aliweza kusomesha watoto wake wote kwa ngazi nzuri za kielimu na kuwakuza katika maadili ya kidini, umoja na upendo kwa watoto wake wote.

Mzee Samuel Musika amekuwa mtu wa mfano wa kuigwa wilayani kwake kwa kutokubagua jinsia ya watoto katika malezi na hata suala la elimu, Kwa miaka ya 1930 hadi miaka karibu na 2000, watoto wa kike ilikuwa ni bahati sana kusomeshwa kwani wao waliandaliwa kwa ajili ya kuolewa kitu kilichokuwa tofauti nyubani kwa Mzee Samuel.

Kwa malezi waliyopewa watoto wake, pia wameonyesha mfano kwa kuwasomesha watoto wao na kuwakuza imara katika dini wengi wao wakiwa ni wa imani ya dhehebu la Seventh Day Adventist Church (SDA) na baadhi ya watoto na wajukuu zake wameshika nafasi mbalimbali kanisani.

Mzee Samuel Musika alifanikiwa kusafiri mikoa na nchi mbalimbali Duniani kutembelea watoto wake, hii ikiwa ni moja ya faida ya kusomesha vyema watoto wake na kuwalea katika upendo na umoja.

Mzee Samuel Musika alifariki tarehe 06/08/2020 nyumbani kwa binti yake katika kijiji cha Nyamuswa wilayani Bunda kwa ajili ya uzee akiwa na umri wa miaka 102 na kuzikwa nyumbani kwake Bukama, Ikizu, Bunda mkoani Mara.

Mke wa Mzee Samuel Musika aliebaki ni mmoja aitwae Nyawanzagi

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

31.59.83.86 20:55, 22 Januari 2016 (UTC)[jibu]