Majadiliano ya mtumiaji:G.J.Kingodo

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

kompyuta[hariri chanzo]

kifaa

Ng'ombe[hariri chanzo]

Ng'ombe (kutoka Kireno "gumbe") ni wanyama wakubwa wanaokula nyasi. Ni wanyama wanaofugwa kwa wingi sana kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi au pia kwa kuvuta plau au gari la kukokotwa.

Kibiolojia ni wanyama wa jenasi Bos. “Ng'ombe-kaya” ni aina zifugwazo za “ng'ombe-mwitu” (Bos primigenius).

Kwa asili kuna aina mbili za ng'ombe-kaya: ng'ombe wa Ulaya na ng'ombe wa Uhindi ambazo ni nususpishi za B. primigenius (B. p. taurus na B. p. indicus mtawalia, ingawa mara nyingi nususpishi hizo zinaainishwa kama spishi za B. taurus na B. indicus). Zinatoka kwa nususpishi za zamani B. p. primigenius na B. p. namadicus.

Siku hizi ni vigumu kufahamu nususpishi za ng'ombe, kwa sababu takriban aina zote za ng'ombe ni chotara sasa.

Ng'ombe hula nyasi na kutembea kwa vidole viwili. Ng'ombe waliofugwa na binadamu walitokana na ng'ombe-mwitu ili kujipatia nyama na maziwa. Katika nchi nyingi hutumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.

Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga na kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.

Ng'ombe wanapatikana kote duniani na kuna aina kwa kila namna ya hali ya hewa. Wengine huishi katika milima baridi za Uskoti na Skandinavia, wengine katika joto la Afrika au Australia.

Wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanairudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. Kwa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nya