Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Edson Nyota

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

EDSON NYOTA (EDDIE NYOTA)

[hariri chanzo]

EDSON NYOTA (born 09 june) ni mtangazaji wa redio na Tv , voice over artist, mshereheshaji wa shughuli na muigizaji kutoka Tanzania. Kwasasa ni mtangazaji wa PILIKAPILIKA kipindi cha EAST AFRICA REDIO na sauti yake (baritone) inatumika kwenye matangazo mbalimbali ya Simba sports club, Pepsi Tanzania, Uviko 19, CRDB bank n.k, kuanzia mwaka 2018 mpaka sasa.


Nyota anatambulika kama mtangazaji anayefanya vizuri kwasasa Tanzania, mwaka 2021 alisherehesha sherehe ya MR.TANZANIA, na mwaka 2023 alisherehesha tuzo za MAGIC VIBE zilizofanyika Mlimani city Dar es salaam Tanzania.

Amezaliwa Iringa, Tanzania; Nyota alianza kuonesha kipaji chake miaka ya 2018, baada ya sauti yake kutumika kwenye kipindi cha Redio E-FM kinachoitwa Back to the 80’s kilichokuwa kinaruka kila jumapili. Baada ya hapo akasikika kwenye kipindi cha Redio kilichoruka Times FM miaka ya 2019. Sibuka FM alisikika mwaka 2021. Kwa miaka yote hiyo sauti yake imekuwa ikitumika kwenye matangazo mbalimbali ya kibiashara ndani na nje ya Tanzania.

Mwaka 2024, Nyota amekuwa akisikika kwenye kindindi cha PILIKAPILIKA kinachoruka EAST AFRICA REDIO jumatatu mpaka ijumaa muda saa tatu za asubuhi mpaka saa sita mchana, huku sauti yake ikisikika kwenye matangazo ya Uviko 19, Pepsi Tanzania, DCB bank pamoja na kunakilisha sauti (dubbing) AZAM TV, DSTV, STARTIMES.

EARL LIFE

[hariri chanzo]

Edson Nyota alizaliwa Iringa Tanzania 09 june. Alisoma shule ya msingi na sekondari mkoani Iringa baada ya hapo akahamia Dar es salaam, kisha akahamia Tanga kwaajili ya masomo yake ya chuo kikuu, na kisha akaenda morogoro Tanzania kusomea Media.

INFLUENCES

[hariri chanzo]

Mwaka 2023 kwenye interview ya Startimes Nyota alisema amekuwa akivutiwa na watangazaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania, mtangazaji kama DEE SEVEN aliyekuwa akitangaza Kiss fm Tanzania moja ya mtangazaji aliyemvutia sana, Eddo Bashir kutoka Iringa Ebony Fm alitajwa na Nyota kama mtu aliyemvutia, Gadner G habash aliyekuwa mtangazaji wa Clouds fm Dar es salaam, Ian Diallo aliyekuwa akitangaza East Africa Redio, Clemence Nyambudu (Mbudu the Boss) aliyekuwa mtangazaji wa Redio Free Africa ni moja kati ya mtangazaji wa kwanza kumuwashia kipaza sauti Nyota na kusikika redioni.

Kwa nje ya nchi Nyota aliwataja watu kama Dj Target wa BBC one extra redio Uingereza, Treasure tshabalala wa Africa ya kusini, Nick Odiambo wa nchini Kenya bila kumsahau Trevor Noah kwa Africa ya kusini.