Trevor Noah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Trevor Noah
AmezaliwaTrevor Noah
20 Februari 1984 (1984-02-20) (umri 40)
Kazi yakeMchekeshaji, Mtangazi, Muigizaji
Miaka ya kazi2002 - Sasa
Tovuti
treornoah.com

Trevor Noah (amezaliwa tarehe 20 Februari 1984) ni mchekeshaji na mtangazaji wa radio na televisheni kutoka Afrika ya Kusini, maarufu sana kwa utangazaji wake kwenye kipindi cha The Daily Show katika mtandao wa Kimarekani wa Comedy Central tangu Septemba 2015.

Noah alianza maisha yake ya sanaa kama mtangazaji, muigizaji na mchekeshaji nchini Afrika ya Kusini. Ameshika nafasi mbalimbali za utangazaji katika Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC), na alishika nafasi ya pili kwenye msimu wa nne wa Strictly Come Dancing mwaka 2008.

Kuanzia 2010-2011, Noah alikuwa muanzilishi na mtangazaji wa kipindi cha Tonight with Trevor Noah kwenye M-Net na DStv. Uchekeshaji wake umempatia mafanikio kimataifa na kupelekea kutokelezea kwenye vipindi vya mijadala ya usiku vya Amerika na mijadala ya Uingereza.

Disemba 2014. Noah alikuja kuwa mchambuzi wa kimataifa kwenye The Daily Show, kipindi cha habari za dhihaka, Marekani. Mwaka uliofuata, alitangazwa kuwa mrithi wa Jon Stewart, mtangazaji wa siku nyingi sana, na amekuwa mtangazaji mkuu wa The Daily Show tangu Septemba 2015. Mwaka wa 2016, Novemba, alitoa kitabu chake maarufu Born a Crime kinachoelezea maisha yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Trevor Noah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.