Born a Crime

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Born a Crime: Stories from a South African Childhood
MwandishiTrevor Noah
LughaKiingereza
AinaTawasifu
MchapishajiSpiegel & Grau
Tarehe ya kuchapishwa
Novemba 15, 2016
Aina ya MediaChapisho la kitabu chenye kava gumu
Kurasa304
ISBN978-0-399-58817-4

Born a Crime: Stories from a South African Childhood ni jina la kitabu cha tawasifu na ucheshi kutoka kwa mchekeshaji Trevor Noah wa Afrika Kusini. Ndani yake anaelezea maisha yake tangu kuzaliwa, wazazi wake waliochanganya rangi, Mzungu wa Uswizi na mama wa Kixhosa mwenyeji wa Afrika Kusini. Kuzaliwa kwake ilikuwa kosa la jinai wakati wa utawala wa Apartheid.

Katika kitabu anaelezea maisha ya dhiki aliyoishi na mamake, urafiki wa karibu waliokuwa nao, kuishi muda mfupi na kuondoka kwa baba yake. Imani ya dini aliyonayo mama yake na mahusiano yake na fundi magari Abel ambaye baadaye kaja kuwa mumewe na jinamizi kuu la maisha ya mama na mtoto. Kitabu kinaanzia tangu mwanzo tawala za kibaguzi hadi kuondoka kwake na kuja tumaini jipya. Anaelezea katika muundo wa kuchekesha, lakini ni hali halisi ilivyokuwa.

Mapokezi[hariri | hariri chanzo]

Kitabu kimechapishwa mnamo Novemba 2016, Born a Crime[1] kilipokelewa vizuri na wahakiki wa vitabu nchini Marekani.[2][3][4][5] Kitabu kimekuwa nafasi ya kwanza kwa mujibu wa New York Times (kimeuza vyema) na kimepewa heshima kama moja kati ya vitabu bora kabisa cha mwaka na The New York Times, Newsday, Esquire, NPR, na Booklist.[5] Mwanzoni mwa mwaka wa 2017, jina la kitabu lilitumika katika kipindi cha mafumbo cha New York Times Crossword Puzzle.[6]

Uhadithiaji[hariri | hariri chanzo]

Maelezo ya kitabu yanaelezea makuzi ya Noah katika Afrika Kusini ya apartheid. Akiwa zao la kichotara lililotokana na baba Mzungu na mama Mwafrika, hajatosheleza ilivyotakiwa kwenye sera za apartheid zilizowekwa. Hata chini ya apartheid, kulikuwa na shida kwake kubaki salama, kwa sababu wakati huo ilikuwa kosa la jinai ukizaliwa umechanganya rangi kati ya baba na mama (hivyo ndio jina la kitabu).[3]

Sehemu kubwa ya kitabu ni shukrani kwa mama yake mzazi Noah, Patricia Nombuyiselo, ambaye amekulia kwenye kijumba cha nyasi kilichokuwa kinakaliwa na watu 14. Alikuwa mwanamke jasiri mshika dini aliyekuwa na tabia ya kumchukua mtoto wake katika makanisa matatu tofauti kila Jumapili, mkutano wa sala Jumanne, masomo ya biblia Jumatano na siku ya vijana ya kanisa ni Alhamisi, haijalishi hata kama kutakuwa na machafuko mitaani na watu wengi kipindi kama hiki wanakuwa majumbani wamepumzika lakini Bi. mkubwa lazima afike kanisani.[2]


Kuigizwa filamu yake[hariri | hariri chanzo]

Kumbukizi hizi zitatumika kuchezeshwa filamu ambayo ndani yake atakuja Lupita Nyong'o ambaye atacheza kama Patricia, mama yake Noah. Vilevile Nyong'o ata-tayarisha filamu hii na Noah kupitia kampuni yake ya utayarishaji maarufu kama Ark Angel Productions.[7] In March 2018, Liesl Tommy is set to direct the film.[8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Noah, Trevor (15 November 2016). Born a Crime: Stories from a South African Childhood. New York: Spiegel & Grau. ISBN 978-0399588174.  Check date values in: |date= (help)
  2. 2.0 2.1 Kakutani, Michiko. "'Born a Crime,' Trevor Noah's Raw Account of Life Under Apartheid", The New York Times, 2016-11-28. Retrieved on 2017-03-18. 
  3. 3.0 3.1 Darden, Jeneé. "Born a Crime: A Memoir of Love, Hope, and Resistance", Los Angeles Review of Books, Los Angeles Review of Books, 2017-02-18. Retrieved on 2017-03-18. 
  4. Seymour, Gene. "Trevor Noah recalls childhood under apartheid in new memoir", USAToday, Gannett Company, 2016-11-14. Retrieved on 2017-03-18. 
  5. 5.0 5.1 "Born a Crime by Trevor Noah". Penguin Random House website. Penguin Random House. Iliwekwa mnamo 2017-03-18. 
  6. Mahowald, Kyle (2017-02-10). "New York Times Crossword Solution 0210-17". nytcrossword.com website. New York Times. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-20. Iliwekwa mnamo 2017-03-18. 
  7. http://deadline.com/2018/02/lupita-nyongo-born-a-crime-trevor-noah-book-1202298166/
  8. Clement, Olivia (27 March 2018). "Tony Nominee Liesl Tommy to Direct Trevor Noah Biopic Starring Lupita Nyong'o". playbill.com. Iliwekwa mnamo 29 April 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)