Majadiliano ya mtumiaji:Daren jox
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
AFYA
[hariri chanzo]Afya ni mojawapo ya mambo muhimu kwa binadamu tena afya njema, inapaswa binadamu awe na afya njema ili aishi vizuri. Afya njema inahitaji chakula bora na mazoezi pia mazingira bora ya kulala, vitu hivyo binadamu yeyote anapopata huweza kuishi na afya njema na kuepukana na afya mbovu ambayo ni mwanzo wa magonjwa kama kipindupindu na mengineyo mengi ya mlipuko.
Nchi nyingi za kimaskini za kiafrika watu wake wamekuwa na afya mbovu ukilinganisha na watu wa ulaya hii haitokani na umasikini tu bali pi na mwenendo mbovu wa viongozi juu ya swala la afya na ushirikiano wa wananchi pia, Serikali za kiafrika zimesindwa kujenga hospitali za kisasa ilizitoe huduma bora kwa wananchi, Hospitali za kisasa zitasaidia upatikanaji wa afya bora kwa watu wote katika jamii husika.
Afya bora itasaidia ukuaji wa taifa husika, Taifa lenye watu wenye afya litakuwa na kusonga zaidi kimaendeleo kwani watu watafanya kazi zaidi na kwakuwa wana afya njem, Hivyo ni vyema taifa liwe na sera nzuri za afya kwa wananchi wake ili kusaidia upatikanaji wa afya bora
Mashirika mengi yanajitahidi kuboresha sera za afya katika nchi za kiafrika, hii inasaidia kwani mataifa mengi yanajitahidi lakini bado inashindikana kuleta afya bora kwa kila mwananchi shirika la afya duniani WHO ni mojawapo ya mashirika yanayosaidia nchi za kiafrika kusonga mbele katika swala la Afya.
Hospitali bora zitasaidia upatikananaji wa afya bora katikla nchi za kiafrika hasa maeneo ya vijijini ambako swala la afya bora limekuwa ni tatizo, sio tu afya bora bali pia mazingira bora na maendeleo lakini si tu hospitali bora lakini pia ziwe na madawa ya kutosha yatakayokidhi mahitaji ya wananchi wote
Mahitaji ya hospitali maeneo ya vijijini ni makubwa ukilinganisha na mjini hii ni kutokana serikali nyingi kuboresha maeneo ya mjini na sio vijijini ambako ndipo penye shida kubwa, inabibi serikali hizi zigeuze macho na kuangalia upande huu wa vijijini
Mungu tunaomba utusaidie nchi zetu za kiafrika
Miaka ya KK
[hariri chanzo]Ndugu Daren. Asante kwa michango yako. Sasa naomba kwa kila mwaka ambao ulianzisha makala kwake, pia uingize habari, angalao tukio moja au mtu aliyezaliwa ama kufariki mwaka huo. La sivyo, makala hizo za miaka hazitaleta faida kwa msomaji. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 19:00, 13 Februari 2016 (UTC)