Majadiliano:Wilaya, tarafa na kata za Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Maswali kuhusu namna ya kuendelea[hariri chanzo]

a) tuache majina ya makala yatakayoandikwa kuwa "Tarafa ya XYZ" au tuzibadilishe kuwa "XYZ (tarafa)"? Baada ya kubadilisha yote sipendezwi na orodha ya "tarafa ya..." mara nyingi mfululizo. Kwangu mimi ingetosha kwa wilaya.

b) Kwa umla nashangaa kidogo juu ya muundo wa utaratibu huu. Najiuliza kama takwimu niliyotumia inaonyesha kweli tarafa na kata zote? Maana ni wilaya 72 na tarafa kama 220 pekee. Ni kweli wastani ya tarafa 3 kwa wilaya tu? na zaidi kuna wilaya zisizo chache zenye tarafa moja au mbili tu? Pia tarafa nyingi zenye kata 1 pekee?

(Ninashangaa kwa sababu hadi maana sasa nilifikiri (samahani!) ya kwamba Kenya wana uzoefu wa kupanga na kuratibu kushinda Tanzania lakini naona si hivyo; muundo wa utawala huko Tanzania inaeleweka kwangu kabisa - Kenya nashangaa kwa sababu bado sijaelewa jinsi walivyopanga ngazi za utawala hali halisi. Yaani ninaelewa ya kwamba wana ngazi zilezile kama Tanzania ila tu jinsi ngazi hizo zinatekelezwa - ajabu (wilaya yenye kata moja ina maana gani??)

c) hapo najiuliza tutumie majina gani. Yaani kama tarafa ni hasa mji sijui kama inapendeza kuiweka chini ya "tarafa ya Marsabit" - itakuwa ni "Marsabit" pekee kwa mji (na mazingira) halafu "wilaya ya Marsabit". Limuru iwe "Limuru" au "Limuru (mji) badala ya "Limuru (tarafa)".

Sijui wenzangu wanaonaje lakini mimi naona hasa mji - je watu wanajisikia ni "tarafa/division" au ni mji - manisipaa n.k. ? Na tutumie jina gani? --Kipala (majadiliano) 23:18, 27 Machi 2009 (UTC)

Binafsi sijaelewa kitu. Ingawa, nimeangalia kile chanzo cha faili, lakini bado nipo mtrgoni. Labda uanze halafu uonyeshe mfano kisha wengine tutafuata! Lakini orodha yao sio rahisi kama ile ya kwetu! Pole kwa kazi!--Mwanaharakati (Longa) 07:33, 28 Machi 2009 (UTC)

Katiba mpya[hariri chanzo]

Katika katiba mpya ya Kenya inasema kuwa mikoa ilibanduliwa na majimbo yakazinduliwa. Tafadhali rekebisha --Trunzep (majadiliano) 09:39, 4 Julai 2016 (UTC)

Kubatilishwa kwa mfumu wa Mikoa[hariri chanzo]

Baada ya uzinduzi wa katiba mpya ya 2010 ilioanza rasmi kuzingatiwa 2013 Kenya ilibandili mfumo wa Mikoa. Hivi sasa Kenya ina serikali ya Kitaifa na seriakli za kikaunti/kata. Hivi sasa Kenya ina ujumla wa kata 47. Hata hivyo mfumu wa majimbo amboa ulitumika hapo awali bado waendelea kutumika kuchagua wambunge wanaotunga sheria za nchi. Hivyo naonelea ni mwafaka kusahihisha nakala hii --Anjakretfep (majadiliano) 20:09, 10 Juni 2018 (UTC)