Majadiliano:Chombo cha angani
Maneno yasiyo kawaida
[hariri chanzo]Makala hii imehaririwa na mtumiaji:Nyabsino kwa kubadilisha lugha mara kadhaa. Nina wasiwasi kuhusu maneno mbalimbali aliyoleta. Naomba atoe ufafanuzi kuhusu maneno aliyobadilisha. Hii ni hasa maneno kama fasikebu, fasi, wafalki, mwanafasi, fataki.
Sipendi kukamtisha tamaa mwanawikipedia mpya kwa kurudisha mabadiliko haya moja kwa moja lakini nina wasiwasi kama maneno aliyetumia ni kweli lugha fasaha kwa mambo yanayojadiliwa. Kamusi zote ninazoona kama vile KKS, KMM na hasa KAST hazijui maneno aliyoleta kinyume zinaonyesha maneno aliyobadilisha sasa.
Naomba ataje vyanzo vyake. Halafu alirejea "taaluma ya Falaki". Naomba aangalie marejeo katika makala astronomia yanayotaja sababu ya kutotumia tena neno "falaki" kwa fani hii. tunaomba pia aangalie uwepo wa neno "Explorer 1"
Kwa sasa nimelinda makala hii pamoja na mwanaanga Kipala (majadiliano) 09:04, 4 Septemba 2014 (UTC)