Justin Timberlake : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2+) (Roboti: Imeongeza be:Джасцін Тымберлейк
d r2.7.2) (Roboti: Imebadilisha: diq:Justin Timberlake
Mstari 100: Mstari 100:
[[da:Justin Timberlake]]
[[da:Justin Timberlake]]
[[de:Justin Timberlake]]
[[de:Justin Timberlake]]
[[diq:Portal:Justin Timberlake]]
[[diq:Justin Timberlake]]
[[el:Τζάστιν Τίμπερλεϊκ]]
[[el:Τζάστιν Τίμπερλεϊκ]]
[[en:Justin Timberlake]]
[[en:Justin Timberlake]]

Pitio la 21:38, 31 Julai 2012

Justin Timberlake
Justin Timberlake.
Justin Timberlake.
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Justin Timberlake
Nchi Marekani
Alizaliwa 31 Januari, 1981
Aina ya muziki Pop na R&B
Kazi yake Mwanamuziki
Mwigizaji

Justin Timberlake (amezaliwa tar. 31 Januari, 1981 mjini Memphis, Tennessee) ni mwimbaji wa muziki wa pop na R&B kutoka nchini Marekani. Timberlake alianza kujipatia maarufu baada ya kucheza kipindi cha televisheni (Mickey Mouse Club) kilichokuwa maalum kwa ajili ya watoto, na baadaye katika kuwa kama mmoja wa washindi wa tuzo ya Grammy-bendi bora ya vijana *NSYNC. Baadaye alianza kuimba akiwa kama msanii pekee na akafanikiwa kutoa albamu mbili za muziki, Justified na FutureSex/LoveSounds.

Wasifu

Maisha ya awali

Asili ya ukoo wa Timberlake ulikuwa unatokea nchini Uingereza, na familia walikulia katika imani za Kibaptist. Wazazi wake walitengana mnamo mwaka wa 1985 na baada ya hapo, mamake aliolewa tena na mume mwingine, vilevile babake akaowa mke mwingine. Maisha yake yote alikulia mjini Millington, Tennessee, katika mji mdogo wa kaskazini ya Memphis.

Mnamo mwaka 1993, Timberlake akajiunga na Mickey Mouse Club, ni mfululizo wa kipindi cha televisheni kilichoshirikisha wasanii walio wengi vijana. Hiyo ndiyo ikawa mara yake ya kwanza kuonja ladha ya umashuhuri. Na katika kipindi hicho Timberlake alishiriki kuanzia msimu wa sita na saba tu.

Wakati wa maonyesho ya kipindi hicho, Timberlake akakutana na aliyewahi kuwa mpenzi wake (Britney Spears), na wengine alikuwemo Christina Aguilera, na mshirika mwenzake wa katika bendi bwana JC Chasez. Ilivyofika mwaka 1995 kipindi kiliisha, na Timberlake akajiunga na bwana Chasez na washikaji wengine, wakaanzisha kundi la muziki lilojulikana kwa jina la *NSYNC".

Maisha binafsi

Timberlake alianza mambo ya mapenzi akiwa yungali mdogo sana, wa kwanza kuwa nae alikuwa mwanafunzi mwenziye na baada ya hapo mwanamuziki wa pop bi. Veronica Finn, lakini penzi lao halikudumu sana wakaachana pasipo na amani.

Baadaye alianza uhusiano na mwanamzuiki Britney Spears, mara tu walipokutana katika kipindi cha televisheni cha Mickey Mouse Club. Mahusiano hayo yalikuwa gumzo kubwa kwa jamii. Mahusiano hayo yaliisha ghafla mwaka 2002 baada ya Timberlake kumshutumu Spears kuwa anamahusiano ya kimapenzi na mwalimu wa ufundishaji muziki wa ku-densi Bw. Wade Robson.

Kunako mwaka wa 2002, akawa na mahusiano ya kimapenzi na mchezaji wa muziki-mwigizaji Bi. Jenna Dewan, vilevile na mwigizaji-mwimbaji Alyssa Milano. Mnamo mwezi wa Aprili ya mwaka wa 2003, akaanza mahusiano na mwigizaji wa filamu Bi. Cameron Diaz baada ya kukutana katika sherehe za ugawaji wa tuzo za vijana za Nickelodeon Kids' Choice.

Baada ya hapo kukawa na fununu nyingi tu zenye kuelezea kwamba wapenzi hao weshaachana, lakini baadaye kunako tarehe 16 Desemba ya mwaka wa 2006 mnamo siku ya Jumamosi katika kipindi cha televisheni kilichokuwa kinarushwa hewani moja kwa moja nyakati za usiku, Timberlake alithibitisha kwamba wawili hao ni kweli hawana mahusiano tena.

Mnamo mwaka 2007, ilijulikana kwamba Tilmberlake ana mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji wa filamu Bi. Jessica Biel.

Nyimbo na albamu

Albamu alizotoa

  • 2002 - Justified
  • 2006 - FutureSex/LoveSounds

Nyimbo maarufu

Mwaka Nyimbo Albamu
2002
  • "Like I Love You"
  • "Cry Me a River"
  • "Rock Your Body"
  • "Señorita"
Justified
2006
  • "SexyBack" akishirkiana na Timbaland
  • "My Love" akishirkiana na T.I.
  • "What Goes Around...Comes Around"
  • "Summer Love"
  • "LoveStoned"
  • "Until the End of Time"
FutureSex/LoveSounds

Nyimbo alizoshirikishwa

Hii ni orodha ya nyimbo maarufu za Justin Timberlake ambazo alirekodi na wanamuziki wengine:

Filamu alizoigiza

  • Model Behavior (2000)
  • Edison Force (2005)
  • Alpha Dog (2006)
  • Black Snake Moan (2007)
  • Shrek the Third (2007)
  • Southland Tales (2008)

Marejeo

  1. http://www.imdb.com/name/nm0005493/
  2. http://www.gm.tv/index.cfm?articleid=21993
  3. Teaching That Makes a Difference: How to Teach for Holistic Impact

Viungo vya nje