Babeli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16: Mstari 16:
Mataifa ya Kale walikumbuka mji wa Babeli kwa muda mrefu. Kitabu cha [[Ufunuo wa Yohane]] katika [[Agano Jipya]] kilichoandikwa mnamo mwaka [[90]] [[BK]] kinatumia jina la Babeli kama jina la kitendawili kuashiria Roma.
Mataifa ya Kale walikumbuka mji wa Babeli kwa muda mrefu. Kitabu cha [[Ufunuo wa Yohane]] katika [[Agano Jipya]] kilichoandikwa mnamo mwaka [[90]] [[BK]] kinatumia jina la Babeli kama jina la kitendawili kuashiria Roma.


[[Category:Iraq]]
[[Category:Historia ya Iraq]]
[[Category:Babeli]]
[[Category:Babeli]]
[[Category:Mji wa Kale]]
[[Category:Mji wa Kale]]

Pitio la 22:57, 22 Machi 2007

Faili:Detail des Ischtar-Tors von Babylon.jpg
Sehemu ya geti ya Ishtar ya Babeli

Babeli ilikuwa mji wa nyakati za kale katika Mesopotamia. Magofu yake hupatikana karibu na mji wa kisasa wa Al Hillah (Irak) kando ya mto Frati 90 km kusini mwa Baghdad.

Orodha ya wafalme wake ilianza mnamo mwaka 2300 KK. Mfalme mashuhuri wa kwanza alikuwa Hammurabi.

Babeli ilkuwa mji mkuu wa madola mawili makubwa kabla na baada ya kipindi cha enzi ya Ashuri. Kati ya 1770 KK hadi 1670 KK na mara ya pili kati ya 612 KK na 320 KK inaaminiwa ilikuwa mji mkubwa duniani.

Wakati wa Dola la Pili la Babeli mfalme Nebukadreza II alitawala nchi zote kati ya Palestina (Kanaani) hadi Ghuba ya Uajemi. Bustani za kuniginia za Babeli ilikuwa moja ya maajabu saba ya dunia.

Wakati ule jeshi la Babeli liliteka mji wa Yerusalem mwaka 587 KK, kubomoa hekalu ya Suleimani na kuwapeleka Wayahudi hadi Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli.

Mwaka 539 KK Wajemia walivamia Dola la Babeli na kuliteka. Babeli iliendelea kuwa mji muhimu katika Dola la Uajemi. Baada ya ushindi wa Aleksander Mkuu juu ya mfalme Mwajemi Darius III ilikuwa chini ya utawala wa Wagiriki. Aleksander alikufa Babeli mwaka 323 KK katika jumba la kifalme la Nebukadreza.

Mwaka 275 KK Wagiriki walijenga mji mkuu mpya wakawalazimisha wakazi wa Babeli kuhamia huko Seleukia. Hii ilikuwa mwisho wa mji ule mkubwa.

Mataifa ya Kale walikumbuka mji wa Babeli kwa muda mrefu. Kitabu cha Ufunuo wa Yohane katika Agano Jipya kilichoandikwa mnamo mwaka 90 BK kinatumia jina la Babeli kama jina la kitendawili kuashiria Roma.