Isa : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
No edit summary |
||
Mstari 1: | Mstari 1: | ||
Nabii '''Isa''' ni [[mtume]] anayeaminiwa na [[Uislamu|Waislamu]] kama mmojawapo wa mitume |
Nabii '''Isa''' ni [[mtume]] anayeaminiwa na [[Uislamu|Waislamu]] kama mmojawapo wa mitume watukufu wa Mwenyezi [[Mungu]] walioletwa kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu duniani, naye ni miongoni mwa mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahimilivu wao mkubwa: Manabii [[Nuhu]] na [[Ibrahim]] na [[Musa]] na Isa na [[Muhammad]]. Yeye ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili. Kati ya Wakristo anajulikana kwa jina la [[Yesu Kristo]]. |
||
Nabii Isa ni mmojawapo wa 124,000 wa mfululizo wa Mitume na Manabii wa Mwenyezi walioletwa ulimwenguni kuwaletea |
Nabii Isa ni mmojawapo wa 124,000 wa mfululizo wa Mitume na Manabii wa Mwenyezi walioletwa ulimwenguni kuwaletea wanadamu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kuhusu upweke na umoja wake, na kumuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani. Mitume na Manabii hawa wameletwa katika zama mbalimbali na kwa watu, kaumu na umma mbalimbali, na mfululizo huu ulianza na Adamu, baba wa wanadamu wote, hadi Mtume Muhammad akiwa ndiye wa mwisho. |
||
==Kuzaliwa kwake== |
==Kuzaliwa kwake== |
||
Mstari 10: | Mstari 10: | ||
:''Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.'' |
:''Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.'' |
||
Nabii Isa alizaliwa na bibi Maryam kimiujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimtuma Jibrili kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa, alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza |
Nabii Isa alizaliwa na bibi Maryam kimiujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimtuma malaika Jibrili kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa, alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwingine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mamake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba. Huu ni mfano mmoja katika mifano minne ya uumbaji aliyotuonyesha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu alimuumba Adam bila ya baba wala mama, na akamuumba Hawa bila ya mama, na akamuumba Isa bila ya baba, na akaumba wanadamu wote waliobakia kutokana na baba na mama. |
||
==Ujumbe wake== |
==Ujumbe wake== |
||
Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye |
Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahili kuabudiwa kwa haki, na ujumbe huu ndio ujumbe uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kupa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ujumbe wa Mtume Muhammad ambao ndio ulikuwa wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote. Alipokuja alitabiri kuwa atakuja baada yake Mtume ambaye atawafundisha wanadamu ukweli wote na kuwaongoza kwenye haki na kuwaeleza kila wanalolihitaji katika maisha yao. |
||
== |
==Kitabu cha Nabii Isa== |
||
⚫ | Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya uongozi na sharia na hekima kwa wafuasi wao. Katika vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii mbalimbali ni Taurati kwa Nabii Musa, Zaburi kwa Nabii Daudi, [[Injili]] kwa Nabii Isa, na Qurani kwa Nabii Muhammad. Kitabu cha Nabii Isa kiliteremshiwa Wayahudi ambao ndio walengwa wake wa kwanza wa Nabii Isa, kama ilivyothibitishwa na Qurani wakati aliposema: |
||
⚫ | |||
⚫ | Wakristo au Manasara |
||
==Miujiza ya Nabii Isa== |
==Miujiza ya Nabii Isa== |
||
Nabii Isa |
Nabii Isa alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbalimbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa ni kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuhu na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbalimbali. Baadhi ya miujiza ya Nabii Isa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ni kuumba ndege kutokana na udongo, kuponyesha vipofu wakaweza kuona, na kuwaondoshea ukoma wale wenye ukoma, na kuhuisha mtu aliyekufa, na kuwateremshia wafuasi wake chakula kutoka mbinguni ili iwe ni dalili kwao wote. |
||
== |
==Imani ya Kikristo kuhusu Isa== |
||
⚫ | Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya |
||
⚫ | Wakristo au Manasara wanahitilifiana katika imani yao kuhusu Nabii Isa, kwani wengi wanamchukulia kuwa ni Mwana wa Mungu, ni Mungu aliyejifanya mtu, na wachache wanamchukulia kuwa ni Mtume au Nabii tu. Makundi haya yalitofautiana baada ya kuondoka Nabii Isa ulimwenguni na kuwaachia wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada yake, mbali na wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walikuja na fikra na mawazo mengine kuhusu Isa au [[Yesu]] kama anavyojulikana na Wakristo, na baada ya muda waligawanyika makundi mbalimbali. |
||
⚫ | |||
== |
==Kurudi kwa Nabii Isa== |
||
Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa au Yesu atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake |
Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa au Yesu atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake aliyoiacha baada ya kupaa kwenda kwa Mola wake, na haya yanaelezwa katika vitabu vya dini vya Kiislamu na vya Kikristo, lakini wanahitilifiana kuhusu namna na njia aliyoondokea ulimwenguni. Waislamu wanasema kuwa Isa alichukuliwa na Mola wake na kupandishwa kwake mbinguni baada ya Wayahudi kutaka kumuua, na kwa hivyo hawakuweza kumuua wala kumsulubu. Wakristo kwa upande mwingine, wanaamini kuwa aliwahi kusulubiwa na kuzikwa kisha akafufuka siku ya tatu. Muhimu hapa ni kujua kuwa Isa au Yesu atarudi tena duniani kukamilisha kazi yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu. |
||
[[Category:Uislamu]] |
[[Category:Uislamu]] |
Pitio la 10:48, 23 Desemba 2007
Nabii Isa ni mtume anayeaminiwa na Waislamu kama mmojawapo wa mitume watukufu wa Mwenyezi Mungu walioletwa kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu duniani, naye ni miongoni mwa mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahimilivu wao mkubwa: Manabii Nuhu na Ibrahim na Musa na Isa na Muhammad. Yeye ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili. Kati ya Wakristo anajulikana kwa jina la Yesu Kristo.
Nabii Isa ni mmojawapo wa 124,000 wa mfululizo wa Mitume na Manabii wa Mwenyezi walioletwa ulimwenguni kuwaletea wanadamu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kuhusu upweke na umoja wake, na kumuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani. Mitume na Manabii hawa wameletwa katika zama mbalimbali na kwa watu, kaumu na umma mbalimbali, na mfululizo huu ulianza na Adamu, baba wa wanadamu wote, hadi Mtume Muhammad akiwa ndiye wa mwisho.
Kuzaliwa kwake
Habari za kuzaliwa kwake Nabii Isa zinapatikana katika Kurani, surat "Maryamu" (19) kuanzia aya 16 - 35.
- Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mcha Mungu. (Malaika) Akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako ili nikubashirie tunu ya mwana aliyetakasika. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.
- Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
Nabii Isa alizaliwa na bibi Maryam kimiujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimtuma malaika Jibrili kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa, alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwingine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mamake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba. Huu ni mfano mmoja katika mifano minne ya uumbaji aliyotuonyesha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu alimuumba Adam bila ya baba wala mama, na akamuumba Hawa bila ya mama, na akamuumba Isa bila ya baba, na akaumba wanadamu wote waliobakia kutokana na baba na mama.
Ujumbe wake
Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahili kuabudiwa kwa haki, na ujumbe huu ndio ujumbe uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kupa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ujumbe wa Mtume Muhammad ambao ndio ulikuwa wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote. Alipokuja alitabiri kuwa atakuja baada yake Mtume ambaye atawafundisha wanadamu ukweli wote na kuwaongoza kwenye haki na kuwaeleza kila wanalolihitaji katika maisha yao.
Kitabu cha Nabii Isa
Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya uongozi na sharia na hekima kwa wafuasi wao. Katika vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii mbalimbali ni Taurati kwa Nabii Musa, Zaburi kwa Nabii Daudi, Injili kwa Nabii Isa, na Qurani kwa Nabii Muhammad. Kitabu cha Nabii Isa kiliteremshiwa Wayahudi ambao ndio walengwa wake wa kwanza wa Nabii Isa, kama ilivyothibitishwa na Qurani wakati aliposema:
- Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi!
Miujiza ya Nabii Isa
Nabii Isa alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbalimbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa ni kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuhu na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbalimbali. Baadhi ya miujiza ya Nabii Isa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ni kuumba ndege kutokana na udongo, kuponyesha vipofu wakaweza kuona, na kuwaondoshea ukoma wale wenye ukoma, na kuhuisha mtu aliyekufa, na kuwateremshia wafuasi wake chakula kutoka mbinguni ili iwe ni dalili kwao wote.
Imani ya Kikristo kuhusu Isa
Wakristo au Manasara wanahitilifiana katika imani yao kuhusu Nabii Isa, kwani wengi wanamchukulia kuwa ni Mwana wa Mungu, ni Mungu aliyejifanya mtu, na wachache wanamchukulia kuwa ni Mtume au Nabii tu. Makundi haya yalitofautiana baada ya kuondoka Nabii Isa ulimwenguni na kuwaachia wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada yake, mbali na wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walikuja na fikra na mawazo mengine kuhusu Isa au Yesu kama anavyojulikana na Wakristo, na baada ya muda waligawanyika makundi mbalimbali.
Kurudi kwa Nabii Isa
Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa au Yesu atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake aliyoiacha baada ya kupaa kwenda kwa Mola wake, na haya yanaelezwa katika vitabu vya dini vya Kiislamu na vya Kikristo, lakini wanahitilifiana kuhusu namna na njia aliyoondokea ulimwenguni. Waislamu wanasema kuwa Isa alichukuliwa na Mola wake na kupandishwa kwake mbinguni baada ya Wayahudi kutaka kumuua, na kwa hivyo hawakuweza kumuua wala kumsulubu. Wakristo kwa upande mwingine, wanaamini kuwa aliwahi kusulubiwa na kuzikwa kisha akafufuka siku ya tatu. Muhimu hapa ni kujua kuwa Isa au Yesu atarudi tena duniani kukamilisha kazi yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu.