Menofisi
Menofisi | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Menofisi wa Rasi (Lycophidion capense)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 20:
|
Menofisi ni spishi za nyoka za jenasi Lycophidion katika familia Lamprophiidae. Jina lao linatoka kwa nususi kwamba meno yao ni marefu na yamepindika nyuma.
Nyoka hawa ni wafupi. Majike ya spishi kadhaa yanaweza kufika sm 60 lakini madume ni wafupi zaidi na menofisi wengi ni kati ya sm 20 na 45. Kichwa chao ni bapa. Kwa kawaida rangi yao ni kijivu au kahawia na mara nyingi wana madoa.
Menofisi hupumzika mchana katika vishimo. Huwinda usiku na kukamata mijusi kwa meno yao yaliyopindika.
Nyoka hawa hawana sumu na hawaihitaji kwa sababu wanakula mijusi tu. Wakishikwa na watu hawang'ati kwa kawaida, lakini tahadhari kwa sababu nyoka wachimbaji fulani wanafanana na menofisi na hawa hung'ata na huwa na sumu, ingawa hawawezi kuua mtu mzima.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Lycophidion acutirostre, Menofisi wa Msumbiji (Mozambique worlf snake)
- Lycophidion albomaculatum, Menofisi Mabaka-meupe (White-spotted wolf snake)
- Lycophidion capense, Menofisi wa Rasi (Cape wolf snake)
- Lycophidion depressirostre, Menosfisi Pua-bapa (Flat-snouted wolf snake)
- Lycophidion hellmichi, Menofisi wa Hellmich (Hellmich's wolf snake)
- Lycophidion irroratum, Menofisi wa Leach (Leach's wolf snake)
- Lycophidion laterale, Menofisi-misitu Magharibi (Western forest wolf snake)
- Lycophidion meleagre, Menofisi Vidoadoa (Speckled wolf snake)
- Lycophidion multimaculatum, Menofisi Madoadoa (Spotted wolf snake)
- Lycophidion namibianum, Menofisi wa Namibia (Namibia wolf snake)
- Lycophidion nanum, Menofisi Mchimbaji (Burrowing wolf snake)
- Lycophidion nigromaculatum, Menofisi Mabaka-meusi (Black-spotted wolf snake)
- Lycophidion ornatum, Menofisi Maridadi (Forest wolf snake)
- Lycophidion pembanum, Menofisi wa Pemba (Pemba wolf snake)
- Lycophidion pygmaeum, Menofisi Kibete (Pygmy wolf snake)
- Lycophidion semiannule, Menofisi Mashariki (Eastern wolf snake)
- Lycophidion semicinctum, Menofisi Magharibi (Western wolf snake)
- Lycophidion taylori, Menofisi wa Taylor (Taylor's wolf snake)
- Lycophidion uzungwense, Menofisi Pua-nyekundu (Red-snouted wolf snake)
- Lycophidion variegatum, Menofisi Tilatila (Variegated wolf snake)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Menofisi tilatila
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Menofisi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |