Luvironza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Luvironza ni jina la mlima mkubwa wa Burundi na pia jina la mto mwenye chanzo chake huko mlimani.

Mlima Luvironza una kimo cha 2,700 m juu ya UB uko kilomita 45 upande wa mashariki wa Ziwa Tanganyika.

Mto Luvironza unaanza hapo ambao hutazamiwa kuwa ni chanzo cha Nile. Mto huu una mwendo wa 110 km hadi kuishia katika mto Ruvuvu ambao ni tawimto wa Kagera.