Luke Shaw

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Luke Shaw mwaka 2015.

Luke Paul Hoare Shaw (aliyezaliwa Julai 12, 1995) ni mchezaji wa soka wa Uingereza ambaye anacheza katika klabu ya Ligi Kuu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza.

Mwanzoni mchezaji huyu alikuwa akichezea klabu ya Southampton, Shaw alicheza katika timu yake ya Southampton kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2012. Mnamo Juni 2014, Shaw alisainiwa na Manchester United kwa ada ya £ 30 milioni.

Tarehe 5 Machi 2014, aliifanya timu yake ya kimataifa ya Uingereza kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Denmark, na baadaye mwaka huo alichaguliwa katika kikosi cha Kombe la Dunia la FIFA.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Luke Shaw kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.