Nenda kwa yaliyomo

Luka Modric

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Luka Modrić (2020)

Luka Modrić, (kwa Kiserbokroatia: [lûːka m⁵ǒːdrit͡ɕ]; alizaliwa tarehe 9 Septemba 1985). Anacheza Hispania klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Croatia.

Anacheza nafasi ya kiungo wa kati na pia anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji au kiungo mkabaji.

Alizaliwa Zadar na alisajiliwa na Dinamo Zagreb baada ya kuonesha uaminifu kwenye timu yake ya mtaani.Alipata maendeleo kwenye ya Zagreb na baadaye kusajiliwa Zrinjski Mostar na baadaye Inter Zaprešić. Alipata mafanikio makubwa akiwa Dinamo na kubeba mataji ya ligi kuu matatu mfululizo na baadaye kuhamia Premier League akiwa na Tottenham Hotspur na ndiye aliyechangia kwenye ushindi wa mara ya kwanza wa UEFA Champions League baada ya miaka hamsini,ambako mara ya mwisho ilfika robo fainali mwaka 2010-11.

Baada ya msimu wa 2011-12 alihamia Real Madrid kwa ada ya £33 milioni chini ya kocha Carlo Ancelotti.Na alifanikiwa kushinda taji la La Décima na kuchaguliwa kua mchezaji bora wa msimu.Kwenye msimu wa 2016 na 2017 alishinda taji la UEFA Champions League kwa mara ya pili na ya tatu,na mwaka 2016 alishinda tuzo za La Liga kuwa ndiye kiungo bora wa mwaka kwa mara ya pili.

Aliweka tena heshima kwenye timu ya taifa dhidi ya Argentina machi 2006 na alishiriki mashindano yote makubwa ambayo Croatia imeshiriki kama vile FIFA World Cup 2014.Alishinda goli lake la kimataifa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia.

Modrić anajumuishwa kati ya wachezaji wazuri wa dunia na ni mchezaji wa kwanza wa Croatia kujumuishwa kwenye FIFA World XI.Na amejumuishwa tena mwaka 2016.Huwa akichaguliwa kama mchezaji bora wa Croatia mara tano nyuma ya Davor Šuker ambaye amechaguliwa mara sita.