Nenda kwa yaliyomo

Gude

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lobotos)
Gude
Gude kijivu
Gude kijivu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Campephagidae (Ndege walio na mnasaba na gude)
Jenasi: Campephaga Vieillot, 1816

Campochaera Salvadori, 1878
Coracina Vieillot, 1816
Hemipus Hodgson, 1845
Lalage Boie, 1826
Lobotos Reichenbach, 1850
Pericrocotus Boie, 1826
Pteropodocys [[]],

Gude au gudegude ni ndege wa familia Campephagidae. Spishi nyingi zina rangi ya kijivu na nyeupe tu na pengine nyeusi, spishi nyingine zina rangi kali pia kama nyekundu na njano. Hawa ni ndege wa misitu isipokuwa gude-ardhi wa Australia ambaye atokea maeneo wazi yenye miti michache. Chakula chao kuu ni viwavi (kwa sababu ya hiyo huitwa “mlaviwavi” kwa lugha nyingi) lakini wadudu wengine pia na pengine wanyama wadogo, matunda na mbegu. Hujenga tago lao kwa umbo la kikombe mtini na jike huyataga mayai 3-4 yenye rangi ya nyeupe, majani au buluu.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]