Nenda kwa yaliyomo

Liubomyr Huzar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha yake.

Liubomyr Huzar, M.S.U. (alizaliwa 26 Februari 193331 Mei 2017) alikuwa Askofu mkuu kabisa wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina, wa kwanza kuchaguliwa nchini Ukraine huru. Alikuwa pia kardinali wa Kanisa Katoliki. Alihamisha kiti cha Lviv kwenda Kyiv mwaka 2005. Mnamo Februari 2011, alistaafu kutokana na matatizo ya kiafya.

Alizaliwa katika jiji la Lwów (sasa Lviv, Ukraine),[1] katika familia ya Yaroslav Huzar na Rostyslava Demchuk (Demczuk)..[2] Luka Demchuk (Demczuk), ambaye alikuwa kuhani wa Parokia ya Ufufuo katika kijiji cha Kal'ne kuanzia mwaka 1909 hadi 1929, alikuwa babu wa mama wa Kardinali Liubomyr Huzar.

Huzar alihama na wazazi wake mwaka 1944 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia kutokana na kuwasili kwa Jeshi la Kisovyeti. [3] Hapo mwanzo, familia ya Huzar waliishi kwa muda mfupi huko Salzburg, Austria, kisha wakahamia Marekani mwaka 1949.[4]

  1. "Greek Catholic Church. Stanislau (Stanislau). Metrical books, 1783-1931. Volume 631-1/707 Births 1890-1901". Family Search.
  2. "Ростислава Олександра Демчук (Гузар) b. 3 мај 1904 d. 23 август 1992 - Родовид". sr.rodovid.org. Iliwekwa mnamo 9 Mei 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Лука Демчук b. 1873 d. 6 март 1929 - Родовид". sr.rodovid.org. Iliwekwa mnamo 9 Mei 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "A Church that was supposed to disappear". Zenit News Agency. 15 Novemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.