Limpopo (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mto wa Limpopo
Mto wa Limpopo mwaka 2000
Chanzo Milima ya Witwatersrand katika Gauteng nchini Afrika Kusini
Mdomo Bahari ya Hindi
Nchi Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe na Msumbiji.
Urefu 1,600 km au 1,800km
Kimo cha chanzo takriban 1,700 m
Tawimito Krokodil, Marico, Olifant
Mkondo 800 m³/s
Eneo la beseni 414,524 km²

Limpopo ina chanzo chake katika mto wa Krokodil (Kiafrikaans: mamba) katika milima ya Witwatersrand kati ya Pretoria na Johannesburg nchini Afrika Kusini. Inapita mwendo wa pinde kubwa ikielekea kwanza kaskazini-magharibi halafu mashariki hadi Bahari Hindi.

Baada ya kupokea mto wa Marico huitwa kwa jina Limpopo. Baadaye inafuata mpaka kati ya Afrika Kusini na Botswana halafu mpaka wa Afrika Kusini na Zimbabwe.

Tawimto mkubwa ni mto wa Olifant (Kiafrikaans: tembo) unaojiunga na Limpopo katika Msumbiji 200km kabla ya mdomo wake. Moto unafikia Bahari Hindi kwa mji wa Xai-xai.

SouthAfricanStub.png Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Limpopo (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.