Nenda kwa yaliyomo

Lilias Armstrong

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lilias Eveline Armstrong
Amezaliwa (1882-09-29)29 Septemba 1882
Pendlebury, Lancashire, England
Amekufa 9 Desemba 1937 (umri 55)
North Finchley, Middlesex, England
Elimu B.A., University of Leeds, 1906
Ndoa Simon Boyanus (m. 1926) «start: (1926-09-24)»"Marriage: Simon Boyanus to Lilias Armstrong" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Lilias_Armstrong)

Lilias Eveline Armstrong (29 Septemba 18829 Desemba 1937) alikuwa mwanafonetiki wa Uingereza.

Alifanya kazi katika chuo kikuu cha London, ambapo alipata kiwango cha msomaji.[1]Armstrong anajulikana zaidi kwa kazi yake juu ya intonation ya Kiingereza pamoja na fonetiki na tani za Kisomali na Kikuyu. Kitabu chake kuhusu intonation ya Kiingereza, alichoandika kwa ushirikiano na Ida C. Ward, kilikuwa chapishoni kwa miaka 50. Armstrong pia alitoa baadhi ya maelezo ya awali ya kina kuhusu tani katika Kisomali na Kikuyu.

Armstrong alikulia Kaskazini mwa Uingereza. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Leeds, ambako alisomea Kifaransa na Kilatini. Aliwahi kufundisha Kifaransa katika shule ya msingi kwenye vitongoji vya London kwa muda, kisha akajiunga na Idara ya Fonetiki ya Chuo Kikuu cha London, iliyokuwa ikiongozwa na Daniel Jones. Kazi zake mashuhuri zaidi zilikuwa ni kitabu cha mwaka 1926 A Handbook of English Intonation alichokiandika kwa kushirikiana na Ward, makala ya mwaka 1934 "The Phonetic Structure of Somali", na kitabu The Phonetic and Tonal Structure of Kikuyu, kilichochapishwa baada ya kifo chake mwaka 1940, baada ya kufariki kutokana na kiharusi mwaka 1937 akiwa na umri wa miaka 55.

Alikuwa mhariri mdogo wa jarida la International Phonetic Association linaloitwa Le Maître Phonétique kwa zaidi ya muongo mmoja, na alisifiwa sana katika kipindi chake kwa ufundishaji, akiwa darasani wakati wa muhula na pia kwenye kozi za likizo za majira ya joto za idara hiyo. Jones aliandika kwenye wasifu wa kumbukumbu yake kwamba alikuwa "miongoni mwa wanafonetiki bora zaidi duniani".

  1. Jones, Daniel (1963). Everyman's English Pronouncing Dictionary (tol. la 12th). London: Dent. uk. xxix; Windsor Lewis, Jack (1985). "British Non-Dialect Accents". Zeitschrift für Anglistik und Amerikanistik. 33 (3): 248. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2017.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lilias Armstrong kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.