Laurenti Company

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Laurenti Company, O. de M. (El Puig, Hispania, 1415 - El Puig, 20 Desemba 1479) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki ambaye mwaka 1452 alikwenda Tunisia kukomboa watumwa.

Wakati wa kurudi, meli ilipatwa na dhoruba: wengi walikufa maji, waliobaki wakarudishwa Tunisi wakafanywa watumwa tena pamoja na Laurenti.

Baada ya miaka 15 aliachiliwa akarudi kwao akafanywa mkuu wa shirika.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Desemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.