Lango:Afrika/Makala iliyochaguliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala iliyochaguliwa[hariri chanzo]

Makala iliyochaguliwa kwa Machi 2012[hariri chanzo]

Eratosthenes

Eratosthenes wa Kirene (Kigir. Ερατοσθένης ο Κυρηναίος, 276 KK - 194 KK) alikuwa mtaalamu wa hisabati, jiografia, historia na lugha na mkurugenzi wa maktaba ya Aleksandria katika Misri. Anakumbukwa hasa kama mtu wa kwanza aliyekadiria mzingo wa dunia. Anasemekana aliibuni neno la jiografia. Erastothenes alizaliwa mnamo mwaka 276 KK mjini Kirene wa Libya. Kirene ilikuwa moja ya miji iliyoundwa na Wagiriki wa Kale huko Afrika. Alienda Athens kwa masomo yake alipofundshwa na wanafalsafa na wataalamu mashuhuri. Mnamo mwaka 255 alihamia Aleksandria iliyokuwa mji mkuu wa Misri. Akawa mwalimu wa mwana wa mfalme na mwaka 236 KK alikuwa mkurugenzi wa tatu wa maktaba ya Aleksandria iliyokuwa kitovu cha elimu cha kimataifa kwa sababu ya mkusanyiko mkubwa wa vitabu.