Lambo la Manchira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lambo la Manchira limeunda bwawa katika Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, Tanzania. Bwawa hili lilijengwa kwa madhumuni ya kusambaza maji safi na salama ya kutosha kwa wakazi wa mji wa Mugumu na vijiji jirani vya Kebosongo, Rwamchanga, Morotonga, Bwitengi, Kisangura na Matare.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ujenzi wa lambo la Manchira ulianza mnamo 1980. Mradi huo mwanzoni ulikadiriwa kugharimu TZS 32m/-.

Tarehe 2 Julai 2010, rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alizindua rasmi bwawa hilo. Mradi huo ulichukua miaka 30 kukamilika na uligharimu taifa zaidi ya TZS 10bn.