Nenda kwa yaliyomo

Lada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiwanda cha magari cha AvtoVAZ huko Togliatti, Urusi mnamo 2010.

Lada (Kirusi:Лада) ni aina ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya serikali ya Urusi AutoVAZ.

Hapo awali, magari hayo yalitolewa kwa jina la "Zhiguli" (Жигули) katika soko la ndani la Umoja wa Kisovyeti. Magari yaleyale yalitolewa kwa jina "Lada" yakikusudiwa kuuzwa nje ya nchi kuanzia 1973. Kimsingi Zhiguli na Lada za kwanza zilikuwa nakala za Fiat 124, na kiwanda kilitengenezwa kwa msaada wa kampuni ya Fiat kutoka Italia.

Baada ya mwisho wa Umoja wa Kisovyeti, Lada iliendelea kuwa chapa kuu kwa masoko yote ya ndani na nje ya nchi.

Baada ya kampuni ya Kifaransa ya Renault kununua asilimia 26 za hisa za AutoVaz, uzalishaji wa magari ya Lada ulisimamiwa na mameneja kutoka Renault kuanzia mwaka 2016.

Baada ya uvamizi wa Ukraine na Urusi Renault ilijiondoa katika uzalishaji wa Lada na kuuza hisa zale.

Mnamo 1993, TTS, iliyoanzishwa mnamo 1992 na Vyacheslav Zubarev, ilisaini mkataba na AvtoVAZ. Mnamo 1995, kituo cha kwanza kamili cha magari Lada kilifunguliwa katika jiji la Naberezhnye Chelny na kuanza uwasilishaji wa moja kwa moja kutoka kwa mmea wa magari. Mnamo 1995, ofisi ilifunguliwa huko Kazan. Hadi 1997, magari yaliendeshwa Kutoka Naberezhnye Chelny.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lada kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.