La Masia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
La Masia.

La Masia de Can Planes (kwa kawaida hufupishwa kuwa La Masia) ni chuo kinachokuza vipaji vya vijana wakiwa bado wadogo katika timu ya FC Barcelona.

Chuo hiki kina wachezaji wadogo zaidi ya 300, na imekuwa sifa tangu 2002 kama chuo bora zaidi duniani, ni jambo muhimu katika mafanikio ya FC Barcelona.

Mnamo 2010, La Masia ikawa chuo cha kwanza kwa vijana kwamba kimefundisha vijana na mwisho wakawa wachezaji bora wa dunia (Ballon d'Or) wachezaji hao ni Andres Iniesta, Lionel Messi na Xavi.

La Masia pia ni jina la mafunzo ya soka ya FC Barcelona, Awali chuo hicho kipo karibu na Camp Nou katika wilaya ya Les Corts. Mfano wa wachezaji wakubwa waliokuzwa na chuo cha La Masia ni Xavi, Andreas Iniesta, Lionel Messi, Carles Puyol, Cesc Fàbregas, Jordi Alba, Sergio Roberto, Sergio Busquets, Pedro, Pep Guardiola na wengine wengi.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu La Masia kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.