Kyelele

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kyelele ni kijiji ambacho kipo katika Kyerwa mkoa wa Kagera, Tanzania.

Hii sehemu ina sifa nyingi: hizo sifa zimeifanya kuwa sehemu ya mvuto. Sifa hizo ni:

1\ Iko karibu na Game Reserve ya Rumanyika: hii imekiletea kijiji hiki hali ya hewa nzuri; mvua hunyesha mwaka mzima. Hii mvua imeweza kuwapa mavuno mazuri. Mazao ambayo hupandwa ni kama vile maharage, mahindi, ndizi, kahawa na kadhalika.

2\ Iko karibu na mto. Huo mto huitwa mto Chigeya na umeiletea maendeleo maana watu wa sehemu hiyo huutumia kupikia pombe ambayo huweza kuuzwa ili kujikimu mahitaji yao kama vile kusomesha, kupata mavazi na kadhalika.

3\ Ina migomba mingi. Watu wa sehemu hii hula ndizi kama chakula mama, kwa hiyo migomba huzalisha ndizi ambayo hutumika kama chakula.

4\ Ardhi yenye rutuba. Hii sehemu katika Tanzania hakika imejaliwa. Watu wa sehemu hiyo hutumia vizuri maana huweza kulima mazao mengi,

Kuna pia matatizo yanayokikumba kijiji hiki, kama: 1\ ukosefu wa barabara 2\ ukosefu wa shule ya sekondari 3\ kuingiliwa na wanyama kutoka kwenye Game reserve 4\ kutopata huduma nyingi za kijami

Ila hiki ni kijiji kizuri cha kuwekeza katika mambo mengi, kama vile ukulima wa kahawa, kwa sababu mvua hunyesha kwa misimu miwili, jinsi ambavyo kahawa huhitaji.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kyelele kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.