Kwentui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwentui ni eneo katika mlima wa Maduda huko Bumbuli, Tanzania, ambalo wakazi wa Bumbuli huenda kuabudia wakati wa majira ya kukumbuka kupaa kwa Yesu Kristo wa Nazareti karibu miaka 2000 iliyopita.

Neno Kwentui limetokana na neno Ntui. Ntui ni neno la Kisambaa ambalo lina maana mbili, kwanza ni kilele cha mlima, maana ya pili ntui hujulikana kama kinu cha asili cha kusagia nafaka kama mahindi, mtama n.k.