Nenda kwa yaliyomo

Kinu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majani yapondwa katika kinu; kwanza yagandishwa kwa njia ya naitrojeni ya kiowevu halafu kupondwa kwa mchi kuwa unga

Kinu ni chombo cha kusaga au kuponda vitu kwa msaada wa mchi vinavyohitaji kusagwa kwa mfano vyakula au madawa.

Kwa asili kinu ni kifaa kinachotengenezwa kwa kutumia miti migumu ambapo gogo hutobolewa sehemu ya juu katikati kuelekea chini ambapo upana wa tundu hupungua kuelekea chini tundu hilo hutumika kuwekea vitu vinavyohitaji kusagwa.

Kinu hutengenezwa pia kwa kukata jiwe kuwa na umbo linalotakiwa pia kwa metali au kauri.

Ili kinu kikamilike huhitaji mchi ambao hutumika kusagia vitu vilivyowekwa ndani ya kinu.

Kinu hutumika katika makabila mengi ya Afrika Mashariki, mifano ipo kama kinu cha Warangi.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kinu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.